Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hizo 4G zenu zitawatokea puani

Wachezaji wa Yanga.

Muktasari:

  • Kocha huyo amewaambia mastaa hao kwamba kejeli zinazoendelea siyo nzuri lakini kinachotakiwa ni kuongeza nguvu kwenye ligi na kutoa kipigo cha maana pamoja na kukusanya pointi kwa kila mmoja anayetokea mbele wakianzia na Majimaji leo Jumanne.

KEJELI za kuwatania Yanga 4G zimemfikia Kocha wao, George Lwandamina. Lakini amezungumza na wachezaji mbalimbali wa kikosi cha kwanza cha timu hiyo na kutafsiri kwa kina kilichotokea Zanzibar na kuwekeana mikakati mipya.

Kocha huyo amewaambia mastaa hao kwamba kejeli zinazoendelea siyo nzuri lakini kinachotakiwa ni kuongeza nguvu kwenye ligi na kutoa kipigo cha maana pamoja na kukusanya pointi kwa kila mmoja anayetokea mbele wakianzia na Majimaji leo Jumanne.

Mmoja wa wachezaji wa Yanga ameiambia Mwanaspoti kwamba kocha huyo amewapa somo la kina na kila mmoja kwa sasa amerudisha akili yake kwenye ligi tayari kwa mapambano na wanamaanisha wanachokisema.

Lwandamina amekerwa na utani wa Simba wanaoiita Yanga 4G wakiwakejeli kwa matokeo ambayo Yanga waliyapata mbele ya Azam FC kwenye Kombe la Mapinduzi ambapo walifungwa mabao 4-0 kwenye hatua ya makundi kabla ya kufungwa kwa mikwaju ya penalti 4-2 na Simba kwenye nusu fainali.

Mastaa wa Yanga wamepigwa mkwara mzito na Lwandamina kuwa hataki kuona wanapoteza pointi hata moja katika mechi 12 zilizobakia.

Mechi za wiki hii ni mwanzo wa mtego wa Simba na Yanga kujaribu kuweka hesabu zao sawa katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu Bara.

Simba ambao ndio vinara wa ligi kuu wakiwa na pointi 44 wanakutana na mtihani wao wa kwanza katika duru la pili dhidi ya Mtibwa Sugar mchezo ambao kama watapoteza watakuwa wameiweka rehani nafasi yao hiyo ya ubingwa.

Ikumbukwe kwamba Simba ina mechi tano katika viwanja vya nje ya Dar es Salaam ambapo moja ni dhidi ya Mtibwa hapo kesho Jumatano na nyingine tatu ni dhidi ya Majimaji, Toto Africans, Mbao na Kagera Sugar.

Simba na Yanga zote zimekuwa na presha kubwa kuwa huenda zikapoteza pointi dhidi ya Azam inayoonekana kuimarika hivyo yeyote atakayepoteza pointi leo au kesho atakuwa amejiweka katika nafasi ngumu.

Habari mbaya kwa timu zote ni kwamba Simba itamkosa kiungo wao mshambuliaji Mohammed Ibrahim ambaye hayupo fiti wakati Yanga itamkosa straika wao Donald Ngoma ambaye ni majeruhi.

Benchi la Ufundi la Yanga, lina tambua fika kuwa ushindi dhidi ya Majimaji na mechi zote zilizosalia ndio njia pekee ya kuzima tambo za Simba ambayo mashabiki wake wamekuwa wakisumbua mtaani.

“Yaliyotokea kwenye Kombe la Mapinduzi yameshapita na sasa tunaangalia mbele. Tunacheza na Majimaji katika mechi ambayo tunatambua itakuwa ngumu kutokana na nafasi ambayo wapinzani wetu wapo,”alisema Kocha Msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi.

Majimaji wao wametamba kuwa hawatokuwa tayari kugeuka ngazi ya ubingwa kwa Yanga na wameahidi kuwaongezea machungu ya Kombe la Mapinduzi.

“Tumewaona Yanga kwenye Kombe la Mapinduzi na tumebaini ubora na udhaifu wao. Ni mechi ngumu kwetu ila tunawatahadharisha Yanga kuwa mechi haitokuwa rahisi kwa upande wao,” alisema Kocha Msaidizi wa Majimaji, Habib Kondo.

Kwenye Uwanja wa Azam Complex, kutakuwa na mechi ya kisasi kati ya wenyeji Azam FC na Mbeya City. Ni mechi itakayomrudisha kwa mara ya kwanza mshambuliaji wa Mbeya City, Mrisho Ngassa kwenye Uwanja wa Azam Complex, tangu alipoachana na Azam kimizengwe mwaka 2012.

Mechi hiyo pia itashuhudia kiungo wa Azam FC, Joseph Mahundi akikutana na Mbeya City ambayo aliichezea kwenye mzunguko wa kwanza msimu huu.

Simba na Mtibwa Sugar ni kesho Morogoro. Tangu Desemba hadi sasa, washambuliaji wa Simba wamefunga mabao matatu pekee huku kazi kubwa ya kufumania nyavu ikifanywa na viungo Mohammed Ibrahim na Muzamiru Yassin.

“Mtibwa ni timu nzuri lakini malengo yetu ni kuibuka na ushindi ili tuendelee kubaki kileleni. Tumefanyia kazi mapungufu yaliyojionyesha kwenye Kombe la Mapinduzi ambalo lilikuwa kipimo tosha kwetu,” alisema Kocha Msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja.