Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Balinya asafisha nyota Yanga

Muktasari:

Tangu asajiliwe msimu huu Balinya hakuweza kufunga goli lolote ile katika Ligi Kuu.

MSHAMBULIAJI  wa Yanga, Juma Balinya ameanza kusafisha nyota kwenye Ligi Kuu Bara baada ya kufunga goli lake la kwanza katika mchezo dhidi ya JKT Tanzania unaondelea uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam.

Bao la Balinya linakuwa ni la pili kwa mashindano baada ya kufunga bao lake la kwanza kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Township Rollers.

Katika mchezo huu timu zote zilianza kucheza mpira wa kawaida wa kutokuwa na mipango ndani ya dakika nane.

Dakika 10, Patrick Sibomana aliifungia Yanga bao akipokea pasi ya Deus Kaseke ambaye alipiga mpira katikati ya wachezaji wa JKT Tanzania na mpira kukutana na Balinya aliyeweka wavuni.

Baada ya bao hilo JKT walionesha kutokubali na kuanza kufanya mipango ya kusawazisha kwa kulazimisha mashambulizi kwenda mbele.

Dakika 13, JKT Tanzania ilisawazisha kupitia kwa mshambuliaji wake Adam Adam ambaye aliingia na mpira ndani ya boksi na kupiga shuti lililoenda moja kwa moja wavuni.

Baada ya goli wachezaji wa Yanga walionyesha kutofurahi na walianza kutumia mbinu ya kupiga mipira mirefu kufanya mashambulizi.

Viungo wa Yanga, Mapinduzi Balama na Papy Tshishimbi walikiwa wanahakikisha pasi zao za chini chini zinafika kwa ufasaha.

Dakika 21, Yanga ilipata bao la pili kupitia Balinya baada ya Deus Kaseke kumpigia pasi na kupiga shuti.

Mabeki wa JKT Tanzania, Frank Nchimbi na Damas Makwaya walionekana kupoteana, kuanzia benchi kwa Mohamed Fakhi kulionyesha pengo katika safu ya ulinzi.

Dakika 34, Deus Kaseke alifanyiwa faulo na Michael Aidan nje ya boksi, faulo hiyo ilipigwa na David Molinga na kufunga bao la tatu mpira ukienda moja kwa moja golini.

JKT walipata bao la pili dakika 45 kupitia Dany Lyanga ambaye aliunganisha kwa kichwa krosi ya Adeyum Ahmed.