Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Lusajo aiweka njiapanda Namungo

Mwanza. Kocha wa Namungo Hitimana Thiery amemtaka Reliant Lusajo kufanya uamuzi sahihi kabla ya kuihama klabu hiyo ya wilayani Ruangwa, Lindi.

Thiery alisema mshambuliaji huyo anatakiwa kujiunga na timu ambayo itampa nafasi ya kuendeleza kipaji chake, vinginevyo anaweza kupoteza dira.

Kauli ya kocha huyo imekuja wakati Lusajo akiwa ameweka ngumu kutia saini mkataba mpya baada ya kutofikia mwafaka na Namungo katika mazungumzo ya awali.

Lusajo ambaye anatarajia kumaliza mkataba wake mwishoni mwa msimu huu, amekuwa na mwenendo mzuri na kufikia hatua ya kumezewa mate na Simba, Yanga.

Akizungumza na Mwananchi akitokea Rwanda jana, Thiery alisema Lusajo ni mchezaji mzuri na mwenye uwezo, lakini kama ataamua kuhama msimu ujao lazima awe makini na klabu anayotaka kujiunga nayo.

Alisema mshambuliaji amekuwa chachu ya mafanikio kwa Namungo ikiwamo kuipandisha Ligi Kuu akiwa mfungaji bora wa Ligi Daraja la Kwanza.

“Akienda Yanga au Simba naamini atapata namba kwa sababu anaweza kukaba, kushambulia na kufunga, lakini nimshauri asifanye haraka kama ataona masilahi anayopata Namungo ni sawa na anapotaka kwenda,” alisema Thiery.

Kocha huyo alisema uongozi ulikosea kutompa Lusajo mkataba wa muda mrefu baada ya kucheza kwa kiwango bora katika mashindano ya Ligi Daraja la Kwanza.

“Uongozi ulipaswa kumpa mkataba wa kuanzia miaka miwili kwa sababu huyo ndiye alikuwa mfungaji bora na kuipandisha timu Ligi Kuu, lakini naamini kila kitu kitakwenda sawa” alisema Thiery raia wa Rwanda.

Kocha huyo wa zamani wa Biashara United, alisema hana namna kumzuia Lusajo asiondoke Namungo kwa kuwa soka ndio maisha yake.

Alisema mshambuliaji huyo ana kipaji cha kufunga mabao na amekuwa shujaa wa timu hiyo iliyopanda daraja msimu huu baada ya kucheza kwa kiwango bora.

Namungo imekuwa tishio katika Ligi Kuu baada ya safu yake ya ushambuliaji kuundwa na nyota watatu Blaise Bigirimana, Lucas Kikoti na Lusajo ambao wanawania kiatu cha ufungaji bora.