Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tuisila: Nimewasikia nakuja

WINGA mpya wa Yanga, Tuisila Kisinda amewaambia Yanga kwamba kabla ya wiki hii kumalizika atakuwa ameshatua nchini, lakini akatuma salamu kwa mabeki wa Simba kuwa wajiandae kwa kazi ngumu.

Akizungumza na Mwanaspoti, Kisinda alisema pia ameambiwa na watu wa Yanga kuna kejeli zinaendelea mitandaoni dhidi yao, lakini wataonyesha kazi yao uwanjani.

Staa huyo aliweka wazi kwamba amesaini miaka miwili Jangwani na tayari ameshafanya kikao na bosi wa klabu hiyo, Hersi Said ambaye amempa faili zima la Simba na ushindani baina ya timu hizo.

Kisinda alisema Hersi amemueleza kila kitu kuhusu Simba, lakini akamtaka amnunulie washambuliaji wazuri tu kisha kazi amwachie yeye.
“Nimeongea mengi na bosi Hersi (Said), ameniambia juu ya upinzani wa Simba na Yanga, mimi sijaona shida kubwa, ameniambia kwamba timu kubwa pinzani hapo ni Simba, lakini pia ameniambia kwamba amebakiza kununua washambuliaji tu.

“Nimemwambia kwamba anunue washambuliaji wazuri tu halafu Simba na hata hizo timu zingine atuachie sisi wachezaji tutakutana nao uwanjani,” alisema mchezaji huyo tegemeo wa AS Vita ambaye Yanga imefanya kazi kubwa kumng’oa kikosini.

Kisinda alisema hajawahi kuogopa beki yeyote na kwamba, ana uzoefu wa kupenya ukuta wowote kwani hiyo ndiyo kazi yake.
Alisema amewahi kukutana na Simba na sasa kazi ile anaihamishia Yanga kuhakikisha inachukua mataji.
“Siogopi mabeki, nimekutana na mabeki wengi tofauti na hata hao wa Simba nimekutana nao wananijua kazi yangu, sasa nataka kuileta Yanga,” alisema.
“Nitakuja huko (Tanzania) haraka, nafikiri wiki hii haitamalizika nitakuwa nimeshafika huko kuja kuanza kazi rasmi.”

MUANGOLA KUTUA ALHAMISI

Kiungo Muangola, Carlos Carlinhos amesitisha mkataba wake kwenye klabu ya Jeshi ya GD Interclub nchini humo na atatua Yanga kesho Alhamisi kupiga mzigo.

Mchezaji huyo ambaye ameshafanya mazungumzo mara kadhaa na Yanga amecheza klabu mbalimbali za Angola wakiwemo matajiri Petro de Luanda na rekodi zinaonyesha huwa hachezi zaidi mwaka mmoja kwenye klabu.

Mwanaspoti linajua kwamba Yanga itamsainisha mchezaji huyo kuimarisha safu ya kiungo hata kocha ajaye, Mrundi Kaze Cedrick anamjua vilivyo.

Kwenye mahojiano na Jornal de Angola, Carlihno alisema: “Nilichofanya kwa nchi yangu kinatosha sasa natoka nje kuonyesha uwezo zaidi na ubora wangu.”