Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bocco: Tunawaheshimu Namungo

Muktasari:

Bocco amefanikiwa kutwaa Ngao ya Jamii mara nane ambapo moja  ni akiwa anaitumikia Azam FC na nyingine tatu ni akiwa na Simba

NAHODHA wa Simba, John Bocco amesema kwamba mchezo wa kesho Jumapili dhidi ya Namungo FC kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid utakuwa mgumu ingawa wamejiandaa kupata ushindi
Simba na Namungo zinakutana katika mchezo huo wa Ngao ya Jamii uliopangwa kuanza saa 9.30 alasiri ukiwa ni wa ufunguzi wa Ligi Kuu msimu huu.
Akizungumza katika mkutano na Waandishi wa Habari leo Jumamosi, Bocco amesema kuwa wanatarajia dakika 90 zitakazokuwa na ushindani kutokana na uimara wa wapinzani wao.
"Tunajua tunakutana na timu nzuri ya Namungo ambayo imekuwa ikionyesha ushindani hivyo mchezo hautokuwa rahisi.
"Hata hivyo kwa upande wetu tumejiandaa vizuri na lengo la msingi ni kuifanya timu ifanye vizuri na kutwaa taji hili," amesema Bocco.
Bocco amesema kuwa mbali na kuongeza idadi ya mataji, Simba pia wamepania kupata ushindi katika mechi hiyo ili kuwapa furaha mashabiki wao.
"Tunawashukuru mashabiki wetu ambao wamekuwa wakituunga mkono na kutusapoti kila wakati.
"Tunawaomba wajitokeze kwa wingi kutupa sapoti na sisi wachezaji tutajitahidi kuhakikisha tunapata ushindi," amesema Bocco.
Bocco amesema kuwa ongezeko la wachezaji wapya katika kikosi chao kunaongeza morali na hamasa ya timu na anaamini watatoa mchango mkubwa kuifanya timu hiyo ipate mafanikio.
Wachezaji wapya ambao wamejiunga Simba katika dirisha hili kubwa la usajili ni Larry Bwalya, Chris Mugalu, Bernard Morrison, Ibrahim Ame, Joash Onyango, Charles Ilanfya na David Kameta