Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bocco pekee anatosha Yanga

KIKOSI cha Simba kitawakosa nyota wake wanne kwa sababu mbalimbali kwenye mechi ya watani wa jadi Yanga, ambayo itachezwa Jumamosi Novemba 7, katika Uwanja wa Benjamini Mkapa.

Nyota ambao Simba itawakosa ni Bernard Morrison anatumikia adhabu ya kukosa mechi tatu dhidi ya Mwadui, Kagera Sugar na Yanga kwa kosa la kumpiga ngumi beki wa kati wa Ruvu Shooting, Juma Nyoso.

Mastaa wengine watakao kosekana kwenye mechi hiyo ya kusisimua ni Meddie Kagere mwenye mabao manne aliyeumia msuli, kiungo mkabaji, Gerson Fraga aliyeumia goti na Chriss Mugalu aliyeumia nyonga muda mchache kabla ya kucheza na Tanzania Prison.

Morrison tangu amesajiliwa na Simba alianza vizuri msimu huu kwa kuonyesha makali yake katika mechi ya kirafiki na Vital’O kisha akaenda kuendeleza katika mchezo wa Ngao ya Hisani alipofunga bao la pili na kusababisha penalti ambayo, John Bocco aliyefunga bao la kwanza.

Tangu hapo Morrison amekuwa mchezaji wa kawaida katika kikosi cha Simba kwani hakuonyesha tena makali hayo ambayo alianza nayo msimu na hata kutokuwepo katika kikosi cha kwanza na amekuwa mchezaji wa kuanzia benchi.

Kagere hakuanza msimu vizuri kwa kwa kutokuwepo katika kikosi cha kwanza kwenye mechi mbili, aliporejea amefunga mabao manne na kuwa kinara wa ufungaji katika kikosi hicho, tangu ameanza kucheza soka hapa nchini amekutana na Yanga mara tano na ameifunga mabao mawili.

Kukosekana kwa Kagere kunaweza kuwa ahueni kwa mabeki wa Yanga kwani katika mechi zote alizokuwepo hata kama akishindwa kufunga alikuwa akisumbua muda wote alipokuwa uwanjani, hata katika mchezo wa mwisho walipokutana aliingia kipindi cha pili na alipiga shuti kali ambalo Kipa wa Yanga, Metacha Mnata alilipangua na Mzamiru Yassin kumalizia na kuifungia Simba bao la nne.

Fraga ambaye amekuwa katika kikosi cha kwanza na amecheza kwa maelewano mazuri na Jonas Mkude katika eneo la kiungo mkabaji amekutana na Yanga katika mechi tatu mbili hakucheza na moja alicheza ambayo alikuwa nusu fainali ya kombe la shirikisho (ASFC) na alifanikiwa kufunga bao la kwanza.

Mugalu amesajiliwa na Simba msimu huu na ameitumikia katika mechi sita za kimashindano na za kirafiki ambapo alifunga mabao saba, hajawahi kukutana na Yanga, angekuwepo katika kikosi ndio ingekuwa mara ya kwanza.

Kocha wa Simba, Sven Vandenbroeck ambaye ndio alieleza kukosekana kwa wachezaji hao watatu wenye majeraha na muda ambao watakuwa nje alisema wala hakuna shida kwani ndani ya kikosi chake kuna wachezaji wanaoweza kucheza mechi hiyo na wakafanya kazi kama ambavyo wangefanya mastaa hao.

Sven alisema kuhusu kuwakosa washambuliaji hao wawili kwa ambavyo ameitengeneza Simba msimu huu inaweza kucheza kwa kumtumia mshambuliaji mmoja ambaye anaweza kuwepo, Bocco au wakatumia staili nyingine ambayo nayo inaweza kwenda kufanya vizuri.

“Tunaweza kuanza na mshambuliaji mmoja huku nyuma yake kukawa na viungo ambao wanauwezo wa kufunga kama Luis, Jose, Francis Kahata, Hassan Dilunga, Said Ndemla, Ibrahim Ajibu na wengineo kama ambavyo tulifanya katika mechi nyingi zilizopita,

“Hakuna ubishi mechi ya Yanga ni kubwa ambayo inagusa hisia za watu wengi na unapokuwa na wachezaji wako wote katika kikosi hali ya kujiamini inaongezeka, lakini wanapokosekana wengine inabidi kutumia mbinu mbadala ili kutokwenda kuonyesha madhaifu yoyote na kikosi changu wachezaji wote waliobaki wapo vizuri kwa kazi,” alisema Sven ambaye amekutana na Yanga katika mechi tatu ameshinda moja, ametoka sare moja na kufungwa moja.

KAULI ZA WADAU

Aliyekuwa beki wa pembeni wa timu hiyo, Kasongo Athumani alisema kukosekana kwa mastaa hao, hakuna maana yoyote kwamba timu hiyo inaweza kukosa matokeo, badala yake anamshauri kocha aanze kuwajengea roho yakupambana waliopo.

“Kikosi cha Yanga kina wachezaji wapya ambao kwa asilimia kubwa, sio wazoefu na mechi hiyo, ingawa hiyo sio sababu ya Simba kudharau mchezo huo, ninachotaka kumanisha, waliopo waanze kuwajenga kiakili na wawaamishe kwamba watapata matokeo,” alisema Athumani na aliongeza kuwa.

“Mbona katika mechi ya Mwadui Fc, matokeo yamepatikana bila kuwepo wachezaji hao ingawa kuna nafasi nyingi walikosa za kufunga, wajengewe umakini watamaliza mchezo, kutokana na aina ya mechi inavyokuwa na mambo mengi,” alisema.

Naye straika wa zamani wa timu hiyo, Emmanuel Gabriel alisema Sven mfumo wake wakutumia straika mmoja hauwezi kuathiri sana kukosekana kwa Kagere. “Kagere ni hatari kwakutumia mashambulizi ya pembeni, lakini mwenye kazi ngumu na hatari zaidi ni Bocco ambaye ana mikikimikiki yakucheza kati anakogongana na mabeki wengi na anafunga vile vile, hapa naonyesha inawezekana kupata matokeo nje ya hao ambao wamepata na matatizo.