Chama atia hofu Simba

KIUNGO wa Simba, Mzambia Clatous Chama alishindwa kuendelea na mchezo dhidi ya Kagera Sugar baada ya kuumia kipindi cha pili ambapo nafasi yake ilichukuliwa na Miraji Athuman.
Akizungumza na Mwanaspoti, Daktari wa Simba, Yassin Gembe alisema waliamua kumtoa kwani alionekana kucheza huku akisikia maumivu na baadaye waligundua amepata maumivu ya misuli ya mguu.
Gembe alisema Chama atafanyiwa uchunguzi zaidi hospitalini ili kujua kama amepata shida zaidi ya ile waliyoigundua awali na majibu ya vipimo hivyo ndiyo yatawaongoza kwenye tiba ya mchezaji huyo.
“Kwa namna ambavyo nimemuona Chama uwanjani baada ya kumpatia matibabu ya awali tatizo lake linaweza kumuweka nje ya uwanja kwa muda wa wiki moja hadi mbili ili kupata nafuu kurudi katika hali yake ya kawaida lakini tusilizungumzie sana hilo mpaka hapo atakapotoka hospitali wanaweza kutupa maelezo mengine.”