Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Magori: Hatujui Senzo alipo, ametuzimia simu

Muktasari:

Jana Agosti 9, 2020 Senzo alitangaza kujiuzulu nafasi yake Simba kupitia akaunti zake za mitandao ya kijamii, kisha muda mfupi ikasambaa picha akionekana akisaini mkataba mbele ya viongozi wa Yanga na wa GSM Injinia Hers Said.

MSHAURI Mkuu wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Klabu ya Simba, Mohamed Dewji 'Mo', Crescentius Magori, amemtaka aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo Senzo Mazingisa, kuonyesha busara na kwenda kukakabidhi ofisi kama utaratibu ulivyo.

Jana Agosti 9, 2020 Senzo alitangaza kujiuzulu nafasi yake Simba kupitia akaunti zake za mitandao ya kijamii, kisha muda mfupi ikasambaa picha akionekana akisaini mkataba mbele ya viongozi wa Yanga na wa GSM Injinia Hers Said.

Magori, ambaye ndiye aliachia kijiti kweye nafasi hiyo ya Mtendaji Mkuu wa Simba, kumpisha Senzo amesema yeye ndiye aliyempokea nchini wakati akitokea Afrika Kusini na kumtafutia vibali vya kazi vilivyomfanya kupata haki ya kuishi na kufanya kazi nchini.

Hata hivyo, Magori akizungumza na Wasafi FM, amesema licha ya sintofahamu baina ya Senzo na Bodi ya Wakurugenzi ya klabu hiyo, lakini staili aliyoondoka nayo haijampendeza kwani, hata simu zake zote hazipatikani tangu alipotua Yanga.

"Kulikuwa na mapungufu mengi kati yake na bodi, Simba iliona na kuamini mtendaji kutoka nje ya nchi ni lazima alete kitu cha tofauti.

“Lakini, kilichonishangaza ni namna alivyoondoka, alitakiwa atoe notice na sio kuandika mitandaoni. Hii sio sahihi na baada ya saa mbili tu kashaenda kwa mshindani wetu Yanga, sijapenda hii kitu.

"Mpaka sasa hapatikani na hatufahamu yuko wapi, ana mikataba ambayo ni document (nyaraka) za Simba, awe mstaarabu tu apatikane aje akabidhi mali za Simba halafu aondoke zake akaanze maisha mapya," amesema Magori.

Aidha, Magori amesema Yanga lazima waende Simba kuomba kibali chake cha kazi na makazi ili kikafutwe na kupatiwa kipya.

"Awe muungwana akabidhi ofisi maisha yaendelee, awasiliane na uongozi wa Simba akakabidhi nyaraka, gari ili aendelee na maisha mapya. Changamoto ya kazi yawezekana ameona huko aendako ni sehemu nzuri kwake, kuna vitu vingi anavyo kwani ndiye aliyekuwa mtendaji mkuu," alisema Magori.

Pia, amesema kuwa muda wowote kuanzia sasa Simba itamtangaza bosi wa kuongoza kwenye nafasi hiyo.