Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwakyembe atoa onyo Uwanja wa Taifa kuitwa 'Kwa Mchina'

Muktasari:

 

  • Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ulizinduliwa rasmi mwaka 2007 ukijengwa kutokana na ushirikiano wa pamoja baina ya serikali za Tanzania na China

Dar es Salaam. Serikali imevionya vyombo vya habari na wadau wa michezo ambao wamekuwa wakiuita Uwanja wa Taifa kwa jina la utani la 'Kwa Mchina'

Onyo hilo limetolewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe katika hafla ya uzinduzi wa nembo maalum itakayotumika kwenye Fainali za Afrika kwa Vijana wenye Umri chini ya miaka 17 (AFCON U17) jijini Dar es Salaam leo.

Waziri Mwakyembe alisema siyo vibaya kwa wadau wa soka kuuita Uwanja wa Taifa kwa majina mengine, lakini kutumia jina la nchi nyingine ni kutoitendea haki Tanzania.

"Huu uwanja haujajengwa kwa msaada bali ni fedha za walipa kodi wa Tanzania hivyo nasema ni upuuzi kuuita 'Kwa Mchina' jina ambalo limekuwa likianza kushamiri kwa vyombo vya habari na mashabiki wa soka.

Huwezi kwenda China, India au nchi nyingine ukasikia wanaita vitu vyao Tanzania hivyo sitaki kusikia kuhusu hilo jina na ni bora paitwe kwa Benjamin Mkapa," alisema Dk Mwakyembe.