Dili la Jordan Pickford, Chelsea lafikia patamu

Muktasari:

  • Pickford ni mmoja kati ya makipa walioonyesha kiwango bora msimu huu na hadi sasa anashika nafasi ya pili kwa kucheza mechi nyingi bila ya kuruhusu bao akiwa amefanya hivyo katika mechi 12 za EPL, nyuma ya David Raya.

CHELSEA imeendelea kufanya mazungumzo na kipa wa Everton, Jordan Pickford, 30, ili kumshawishi ajiunge nao dirisha lijalo la majira ya kiangazi kwa ajili ya kuboresha eneo lao lao la beki.

Pickford ni mmoja kati ya makipa walioonyesha kiwango bora msimu huu na hadi sasa anashika nafasi ya pili kwa kucheza mechi nyingi bila ya kuruhusu bao akiwa amefanya hivyo katika mechi 12 za EPL, nyuma ya David Raya.

Kipa huyu amekuwa tegemeo kikosi cha timu ya taifa ya England na timu yake na msimu huu amecheza mechi 40 za michuano yote.

Licha ya uwepo wa Djordje Petrovic na Robert Sanchez, benchi la ufundi la Chelsea limeonyesha kutoridhishwa na viwango vyao, hivyo wanahitaji kufanya maboresho zaidi.

Mkataba wa Pickford unamalizika mwaka 2027 na Everton huenda ikahitaji zaidi ya Pauni 50 milioni kwa ajili ya kumuuza.

CRYSTAL Palace imepanga kumuuza beki wao raia wa  England, Marc Guehi, 23, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi badala ya kumuuza mawinga wao kutoka Michael Olise, 22, kutoka Ufaransa na  Eberechi Eze wa England. Palace imepanga kumuuza Marc mwenye umri wa miaka 23,  badala ya Olise na Eze kwa sababu mchango wao mawinga hao ni mkubwa zaidi ukilinganosha na Marc.

Man United ni moja ya timu zinazohitaji kumsajili.

CHELSEA inaangalia uwezekano wa kumuuza straika wao kutoka Albania, Armando Broja katika dirisha lijalo  la majira ya kiangazi baada ya kumaliza mkataba wake wa mkopo na Fulham. Mabosi wa timu hii wanataka kumuuza staa huyu mwenye umri wa miaka 22, kwa sababu inataka kupunguza gharama za matumizi ya pesa ili kuepuka adhabu kwa kukiuka sheria za matumizi ya pesa.

NEWCASTLE imeripotiwa kufikia makubaliano binafsi na beki wa Bournemouth na England Lloyd Kelly, 25, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi na mkataba wake unamalizika mwisho wa msimu huu. Kelly mwenye umri wa miaka 25, ni mmoja kati ya mastaa walioonyesha kiwango bora msimu huu na amecheza mechi 23 za michuano yote. Mkataba wake unamalizika mwishgo wa msimu huu.

RAIS wa Barcelona, Joan Laporta amewasiliana na Getafe na Manchester United ili kuulizia uwezekano wa kumsajili mshambuliaji Mason Greenwood dirisha lijalo la majira ya kiangazi baada ya kuridhishwa na kiwango bora alichoonyesha tangu ajiunge na Getafe. Staa huyu wa kimataifa wa England akiwa na timu hiyo kwa mkopo msimu huu amecheza mechi 32 za michuano yote na kufunga mabao 10.

MANCHESTER United imetuma wawakilishi wake Jijini Milan kumtazama beki wa Inter Mila, Denzel Dumfries dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Staa huyu mwenye umri wa miaka 28, mkataba wake wa sasa unamalizika mwaka 2025 na hadi sasa mazungumzo ya kusaini mkataba mpya kati yake na Inter yamekwama. Msimu huu amecheza mechi 34 za michuano yote.

NEWCASTLE United na Inter Milan vinamwania beki kisiki wa Barcelona na Ufaransa, Jules Kounde dirisha lijalo la majira ya kiangazi baada ya kuvutiwa na kiwango alichoonyesha tangu kuanza kwa msimu huu. Staa huyu wa kimataifa wa Ufaransa mara kadhaa pia amewahi kuhusishwa na Chelsea, Manchester United na Paris St-Germain.

MSHAMBULIAJI wa AS Roma, Tammy Abraham anataka kurudi Ligi Kuu England dirisha lijalo la majira ya kiangazi na West Ham imeonyesha nia ya kutaka kumsajili. Fundi huyu (26), msimu huu hajaonyesha kiwango bora na amecheza mechi nane za michuano yote na kufunga bao moja. Mkataba wake wa sasa unamalizika mwaka 2026.