Mke wa mtu anataka nimuoe mke wa pili

Muktasari:

3. ANKO Lao, mi nina mpenzi tunayependana sana, ila mwenzangu nikimwambia tukae pamoja hataki, anataka niwe naenda na kurudi kwetu. Nifanyeje?

Jesca Mkalamiti, Ifakara 

1. ANKO Lao, nina demu tunapendana, ila ni mke wa mtu na tumepeana malavidavi hadi kaachika na sasa anataka nimuoe, lakini nami nina mke, japo kasema yu tayari hata awe mke wa pili. Nifanyeje na huu msala?

John Mangelo, Katavi

Jibu: Umekosea sana kwa kuvunja ndoa ya mwenzio, pia kwa kukosa uaminifu kwa mkeo? Kifupi unaonekana hujatulia na huheshimu ndoa kabisa. Kwa vile umeutwanga huna budi kuubwia kwani siku zote mwanakulitafuta...mwanakulipata... Pambana na hali yako!


2. ANKO Lao, nina umri wa miaka 17 kila demu ninayemuona huwa namtamani, lakini naogopa kumwambia. Nifanyeje nisiwe muoga kuwatokea?

Barakael Ernest, Simiyu

Jibu: Kwa umri ulionao ni lazima uchachawe kwa mademu, ushauri itafute kesho yako kwa kukomalia kitabu kama unasoma, hizi ishu za malavidavi bado sana kwako...utajipa presha za bure!


3. ANKO Lao, mi nina mpenzi tunayependana sana, ila mwenzangu nikimwambia tukae pamoja hataki, anataka niwe naenda na kurudi kwetu. Nifanyeje?

Jesca Mkalamiti, Ifakara 

Jibu: Mabinti wa zama hizi mnajirahisi sana, yaani mtu hata hujaolewa tayari unataka kujimilikisha kwa mtu? Ebu oneni aibu kidogo! Kwanini usisubiri uposwe na uolewe, ili uwape heshima wazazi, huoni kama kujipeleka ovyo ni kujitia gundu bure! Alichokifanya jamaa ni sahihi....kajitulize kwenu!


4. ANKO Lao, ninaye mchumba na ninampenda sana, tatizo lake kila nikiomba mzigo ananizingua. Nifanyeje ajue kuwa nampenda?

Petro Makuru, Mwanza

Jibu: Hivi nyie mmerogwa na nani? Yaani uchumba tu, tayari unajiona mume...nampa kongole huyo bibie kwa kukupeleka mswaki...kama unataka kuruka majoka, pambana uoe ili ujilie kwa raha zako!


5. ANKO Lao, binti miaka 19, ninaye mpenzi tunapendana sana, ila ana wivu balaa, nisisimame na mtu kosa, amefikia kuniita danga. Nifanyeje?

Nasra Humud, Rufiji

Jibu: Mwambie jama’ako aache ushamba, hapo hajakuoa wivu upo hivyo akishakuoa huyo si atakuzuia hata kwenda dukani...Ila nini? Maadam ushajua mwenzako ana wivu, epuka kumrusha roho kwa tabia za kusimama na wanaume... Pia kaa naye mueleze tabia yake inavyokukera kwa vile sio kila unayesimama naye ni mtu wako. Asipobadilika ni wewe tu sasa!


6. ANKO Lao, nimepata mpenzi mpya baada ya kutendwa na ma-ex wangu, ila bado sijiamini kama ananipenda kweli. Nifanyeje nijue ananipenda?

Salma Kendra, Tabora

Jibu: Mwanamke kujiamini wewee! Ila ukitaka kujua kama kweli jamaa kakolea au anazuga tu kwako, muombe apeleke posa kwenu ili akuoe. Akikubali ujue huyo wako, mengineyo ni zuga na saundi tu!


7. ANKO Lao, kijana miaka 33 nimeoa, ila sijui kwanini nikiwa na mwenzangu karibu namchukia sana, lakini nikiwa naye mbali nam-misi kinoma. Nifanyeje?

Maduhu Sylvetser, Mwanza

Jibu: Pole sana! Kuna mawili huenda ulimuoa kwa kulazimishwa au hajiweki sopusopu ama unasumbuliwa na pepo baya linalokufanya umchukie mkeo bila sababu. Fanya ibada umuombe Mungu likutoke, pia jenga mazoea na kumtoa outing, itamfanya awe sopusopu na kuvutiwa naye maradufu.


8. ANKO Lao, nina miaka 25, kuna mwanaume naishi na nimezaa naye watoto wawili, ila haonekani kunijali tena kama zamani, sasa nataka kumtoroka nimuachie watoto,  nikatesti maisha mengine. Ni sahihi?

 Aggnes Peter, Ukonga

Jibu: Ulibugi mwenyewe kwa kujirahisisha kwa jamaa kwa kumzalia watoto kabla ya ndoa na hili ndilo linalowaangusha mabinti wengi wa zama hizi. Umefujwa na kupoteza urembo kizembe kwa kuyakimbilia maisha bila ya taratibu. Ila sio ishu sana...kaeni myajenge, nyie ndo pekee mnaoweza kufanikisha mipango yenu kama mpo siriazi. Juu ya kutoroka na kuwaacha watoto sidhani kama ni suluhu...utawatesa watoto bure na usitegemee huko unakotaka kukimbilia kama utatoboa! Hivyo tu!


9. ANKO, kijana miaka 21, kuna demu anakula sana vyangu, lakini hataki kutoa mzigo. Naomba ushauri wako, nifanyaje?

Andrew M.J, Ifakara Moro

Jibu: Mayanki wa zama hizi sijui mnafeli wapi, huwa mnawaingia mademu kindezi ndo maana mnachunwa kiboya. Pia nilichogundua kwako ni kwamba una pesa ya mawazo, halafu una domo zege, hivyo huyo bibie ameshakusoma na kujua we ni joka la kibisa lisilo na madhara kwake. Cha kufanya ni kuchagua kusuka au kunyoa, kwani kwa sasa hauna tofauti na mpenzi mtamazaji tu kwa bibie!


10. ANKO Lao, kijana miaka 23, nimekuwa nikijitahidi kuweka akiba kwa kipato ninachokiingiza kila uchao, ila matatizo hayaishi, nashindwa kufikia malengo. Shida itakuwa ni nini na nifanyeje?

Isaac Makoye, Bunda

Jibu: Tatizo lako una pesa za mawazo, halafu kila unachokipata unakuwa umeshakipigia hesabu kabla ya kukitimia mkononi. Nakupa ujanja, jenga nidhamu ya matumizi kwa kuhakikisha unatumia kidogo na kuweka akiba kingi, naamini utatoboa ila ukiendekeza usemi kwamba tumia fedha upate fedha, basi ujue utaula wa chuya, si unajua maisha yamebana kinoma. Kazi kwako!

11. ANKO Lao, nina miaka 29 kuna kijana ananipenda sana hadi kaachana na mkewe kisa mimi, ila hapendi niongee na simu na ukimpa shida zangu anasema hana hela na kunioa pia hataki. Nifanyeje?

Mwanahamis Kibwana, Tandika

Jibu: Hiyo ndo dhambi ya kumtibulia mwanamke mwenzio, kama hujui nawe utachezewa tu na huyo jamaa kisha akuache kama ulivyo, kwani ni wazi sio mwaminifu ndo maana alimtema mkewe ili awe nawe..akimpata pisi kali zaidi yako atakumwaga vilevile... Ebu shtuka wewee!


12. ANKO Lao, binti miaka 35, nina mchumba tunapendana sana ila anapenda kunywa pombe na kuwa mkorofi akishautwika. Nifanyeje?

Glory Mushi, Arusha

Jibu: We mbibi mzima unajiita binti, hakuna binti wa miaka 35 wewee...inashangaza yaani hadi umri huo umechumbiwa badala ya kuwa katika ndoa?! Kuhusu jama’ako ujue kabisa ana kichwa chepesi ndo maana akipiga ulabu kidogo tu netiweki zinakata na kuanzisha timbwili. Zungumza naye aache kilevi la sivyo mtatemana, kama kweli anakupenda atakusikiliza...! Pia usiache kumuombea abadilike!


13. ANKO Lao, kijana miaka 22, nilikuwa katika uhusiano na binti tuliyeachana naye mwaka jana, ila cha ajabu kwa sasa kila nikilala huwa namuota. Hii inaweza kuwa nini na nifanyeje?

Japhet, Kilwa

Jibu: Ni wazi umemtema huyo bibie, lakini ukiwa bado unampenda na kumweka kichwani ndo maana unamuota kila mara...ushauri wangu Move on... Ila ukiona umeshindwa kushikilia bomba, rudisha majeshi tu ili usije kufa kwa stresi bure, iwapo naye atakuwa bado anakupenda. Hivyo tu!


13. ANKO Lao, kijana miaka 26, nasumbuliwa na tatizo la kusahau vitu, yaani naweza kununua vitu, lakini nasahau mahali nilipoweka na kwenda kununua tena. Nifanyeje?

Masanja Noya, Kiwangwa Bagamoyo

Jibu: Braza kwani unatumia sigara bwege au ni tatizo la kuzaliwa nalo? Kama unatumia hiyo kitu achana nayo inchangia dishi kuyumba. Lakini kama ni tatizo la kimaumbile unapaswa kuwaona watabibu kuweka mambo sawa, pia tumia vyakula vinavyoboresha kumbukumbu kama Lozi (Almondi), Omega 3 na tiba mbadala zitazokuweka fiti, maana tatizo ulilonalo si mchezo. Fanya hivyo!


14. ANKO Lao, nina mpenzi tunapendana sana, ila tatizo lake mwenzangu anakasirika bila mpango kiasi cha kunikera. Nifanyeje aweze kubadilika?

George Dickson, Kigamboni Dar

Jibu: Sijajua umri mlionao, ila ni wazi mmevamia malavidavi katika umri mdogo ndo maana utoto mwingi na mwenzio anashindwa kujikontroo na kukasirika hovyo au kuna mambo asiyopenda kufanyiwa ila wee hubadiliki. Muhimu kaeni chini muweke mambo yenu freshi, la sivyo hamfiki mbali!


15. ANKO Lao, kijana miaka 28, nina mpenzi nampenda sana ila tatizo anapenda sana hela na haridhiki kwani anataka kila siku niwe namtumia, bila kujali ninazo ama la! Nifanyeje?

Gasper Mushi, Moshi

Jibu: Tafuta pesa bro, uache malalamiko, hakuna aliyekutaka ushobokee malavidavi, pia lazima ujue pesa zimeumbiwa mademu na kama una za mawazo ni vyema ukakausha kwanza, si unajua starehe gharama. Hivyo jipange tu kwa vile hata ukimpiga chini huyo bado utaombwa hela tu na mwingine!


16. ANKO Lao, kijana miaka 23, kuna mwanamke naishi naye na tuna miezi minane na nimegundua ni muongo katika mahusiano. Nifanyaje?

Ally Mshana, Arusha

Jibu: Hili ndilo tatizo la kubebana bila hata kujuana vyema tabia zenu, ni wazi nyote sio waaminifu ndo mnachunguzana na siku zote ukimchunguza sana kuku huwezi kumla...kama bado una mipango naye zungumza ili muende sawa, ikishindikana ni wewe tu, kwani hujamuoa, kwanini ujikabe kiboya?


17. ANKO Lao, kijana miaka 18 nina mchumba wangu yupo Morogoro na mimi nipo Arusha, sasa kweli kuna mahusiano hapo?

Hamisi Mbwana, Arusha

Jibu: Kwa umri ulionao ni wazi umekurupukia malavidavi ndo maana umeanza kuchechewa kuwa mbali na demu wako. Ushauri wangu ungepambana kwanza kuitafuta kesho yako, halafu hizo ishu ukaja kushobokea wakati umeshajijenga kimaisha, kwa sasa ni kutaka kujipa stresi za bure bila sababu.


18. ANKO Lao, binti miaka 18 na nina ujauzito ila nikifanya kosa lolote hata dogo tu, mpenzi wangu ananipiga. Nifanyaje?

Mwanaidi Juma, Morogoro

Jibu: We mwana... kiranga gani kilichofanya katika umri huo ukajibebesha mzigo usioumudu? Ila kwa vile ushabugi kwa kutotulia kwenu... vumilia tu. Cha kufanya zungumza na jama’ako anayeonekana ana stresi ili atulie kwani msala aliutaka mwenyewe kwa kutotumia zana. Akiendelea kuzingua mfikishe serikali za mitaa au dawati la jinsi akili zimkae sawa...ukimuendekeza atakudhuru huyu!


19. ANKO Lao, kijana miaka 29 na nina mchumba lakini haonyeshi kama ananipenda, naomba ushauri wako.

MC Kissoi, Chalinze

Jibu: Hivi unajua taratibu za uchumba au unajisemea tu? Unawezaje kuchumbiana na asiyekupenda kama sio kituko! Ila ushauri wangu, zungumza naye ujue moja kama hasomeki jiongeze kwa kutafuta chaka jingine maisha yaendelee...usijikabe kama vile Chalinze nzima pisi kali ipo yeye tu...wewe vipi?


20. ANKO Lao, kijana miaka 24 kuna binti nipo naye katika uhusiano lakini wazazi wake hawataki aolewe kwa sasa. Nifanyeje?

Amir Nditi, Dar

Jibu: Tatizo unaleta usela kwa watoto wa watu, kama ungekuwa siriazi na huyo binti ni wazi ungefuata taratibu za kupeleka posa kwao na kumchumbia... ungefanya hivyo, sidhani kama wakwe wangeleta ukauzu, ila kwa sasa wanabana kwa vile unajiendekeza...! Fanya hivyo uone!