Freddy namba zinambeba Simba

Muktasari:

  • Pamoja na kuwa Simba ina matatizo mengi kwenye kikosi chake lakini ni ukweli usiopingika kuwa eneo la umaliziaji/ushambuliaji ndilo linaongoza kwa kuwa na matatizo ndani ya uwanja kwani timu hiyo imekuwa ikitengeneza nafasi nyingi za mabao lakini imeshindwa kuzitumia vyema licha ya kuwa ina mabao 41 hadi sasa kwenye ligi baada ya mechi 21.

SIMBA baada ya kuchapwa mabao 2-1 na watani wao wa jadi Yanga kwenye mechi ya ligi wikiendi iliyopita, jana ilikuwa uwanjani Zanzibar kwaajili ya michuano ya Kombe la Muungano lililorejea baada ya miaka 20, ila kubwa zaidi ni namna mshambuliaji wake Freddy Michael anavyojitofautisha na wachezaji washambuliaji wengine wa kikosi hicho.

Pamoja na kuwa Simba ina matatizo mengi kwenye kikosi chake lakini ni ukweli usiopingika kuwa eneo la umaliziaji/ushambuliaji ndilo linaongoza kwa kuwa na matatizo ndani ya uwanja kwani timu hiyo imekuwa ikitengeneza nafasi nyingi za mabao lakini imeshindwa kuzitumia vyema licha ya kuwa ina mabao 41 hadi sasa kwenye ligi baada ya mechi 21.

Msimu huu Simba haina mchezaji maalumu wa eneo hilo. Imekuwa ikibahatisha kwa kuwapanga mastaa tofauti kucheza eneo hilo la ushambuliaji lakini wengi wao namba zinawaangusha tofauti na ilivyo kwa Freddy.

Licha ya kuwepo kwa washambuliaji asilia watatu, Freddy na Pa Omary Jobe waliosajiliwa kwenye dirisha dogo lililofungwa Januari mwaka huu sambamba na mkongwe John Bocco ambaye kwa sasa hayuko kwenye timu akifundisha kikosi cha vijana cha Simba, hakuna hata mmoja mwenye nafasi ya kuaminika kuanza mara kwa mara katika eneo hilo ila bado namba zinambeba zaidi Freddy.

Katika mechi za hivi karibuni, benchi la ufundi la Simba limekuwa likimlazimisha Saidi Ntibazonkiza ‘Saido’ ambaye kiasili ni winga kucheza eneo hilo lakini hajawa na matokeo chanya kama ilivyo kwa Freddy akicheza eneo hilo.

Wachezaji wengine wa Simba wanaocheza eneo la ushambuliaji mara kwa mara kulingana na mfumo wa 4-2-3-1 anaoupenda kocha Benchikha ni Kibu Denis, Clatous Chama na Sadio Kanoute ambao pia bado hawajafika anga za Freddy.

Saido hadi sasa amecheza mechi 20 za ligi na kuhusika kwenye mabao tisa, akifunga saba na kutoa pasi za mwisho (asisti) mbili. Hata hivyo katika mabao hayo saba ya Saido, matano ameyafunga kwa mikwaju ya penalti.

Kibu amecheza mechi 19 za ligi na kuhusika kwenye mabao manne pekee akifunga moja na kutoa asisti tatu namba ambazo sio nzuri kwa mshambuliaji anayepata muda mwingi kucheza kama Kibu.

Kwa upande wa Chama yeye ndiye kidogo mwenye afadharli akiwa amehusika katika mabao 13 akifunga saba na kutoa asisti sita katika mechi 19 za ligi alizocheza kiungo mshambuliaji huyo.

Mshambuliaji mwingine aliyefeli ndani ya Simba ni Pa Jobe aliyetua kikosini kwenye dirisha dogo sawa na Freddy. Jobe amefeli kwenye kumshawishi kocha kwani amecheza mechi 11 kwa dakika 281 lakini ameshindwa kuonyesha ubora akiwa amefunga bao moja tu. Mwingine ni Willy Onana ambaye amefunga mabao mawili tu hadi sasa kwenye ligi.

Freddy anawapiga bao wote hao kulingana na muda aliocheza na mabao aliyofunga ambapo hadi sasa amecheza mechi 11 za ligi ambapo nyingi ameingia akitokea benchini lakini kwa ujumla amecheza dakika 431 tu ambao ni wastani wa mechi tano tu kama angecheza kwa dakika 90.

Katika muda huo, Freddy amefunga mabao manne, ikikaribia wastani wa bao moja kwa kila dakika 90 na hadi sasa ndiye mchezaji aliyecheza dakika chache zaidi na kufunga mabao mengi ndani ya Simba.

Mwenendo huo umekuwa mzuri kwa Freddy licha ya ‘kuchukuliwa poa’ na hata alikotoka Green Eagle ya Zambia alikuwa amefunga mabao 14 katika mechi 16 na hadi sasa ndiye kinara wa upachikaji mabao ligi ya Zambia nyumbani kwa kina Chama na Kennedy Musonda.

Katika moja ya mahojiano aliyoyafanya na Mwanaspoti, beki wa Tanzania Prisons, Jamal Masenga aliyewahi kukabana na Freddy alisema ni miongoni mwa washambuliaji hatari aliowahi kuwakaba kwenye Ligi Kuu.

“Ni mshambuliaji mzuri kwani ana nguvu na uwezo mkubwa. Ni ngumu kumkaba. Utofauti wake na washambuliaji wengine yeye ni mtu wa kukaa mbele ya goli na mguso wake wa mpira ni wa tofauti na huwa hatoki kwenye eneo lake kama ilivyo kwa wengine,” alisema Masenga aliyefunguka kuwa usipokuwa makini Fredy anakuadhibu muda wowote.

Mchambuzi wa soka, Ramadhani Mbwaduke alisema kwa namna Simba inavyocheza kwa sasa, ipo haja ya kumuamini Freddy na kumpa muda wa kucheza kikosini hapo.

“Simba imekuwa ikibadili wachezaji kwenye eneo la ushambuliaji lakini takwimu zinambeba zaidi Freddy kuliko Saido na Jobe wanaocheza eneo hilo. Ipo haja ya benchi la timu hiyo kumpa muda wa kutosha Freddy kwani anaweza kufunga na tayari amethibitisha hivyo,” alisema Mbwaduke anayesifika kwa takwimu za soka.

Kocha wa zamani wa Simba ambaye kwa sasa anakinoa kikosi cha timu ya wanawake ya Simba na Taifa Stars, Juma Mgunda alisema Freddy anapaswa kuaminiwa na kupewa muda zaidi atafanya vizuri.

“Tangu mwanzo nilisema Simba kuna presha kubwa sana. Wachezaji wanapojiunga na timu wanakuwa na wakati mgumu wa kuzoea presha lakini kadri siku zinavyoenda wanazidi kuzowea na kufanya vizuri.

“Kwa sasa, Freddy ameanza kuzowea na kurejea kwenye ubora wake, nadhani akiaminiwa zaidi atafanya vizuri na kufunga sana kama alivyokuwa akifanya huko alikotoka,” alisema Mgunda.

RAMADHAN ELIAS