TETESI ZA USAJILI BONGO: Simba yamuwinda Mrundi, Yanga yafuata kiungo jeshini

Muktasari:

  • Simba wanapambana kunasa saini ya staa huyo wa Burundi ambaye ametupia mabao manne kwenye Ligi Kuu Bara iliyotamatika Mai 29 akiwa na Namungo na aliliambia gazeti hili anampango wa kuondoka msimu ukiisha.

UONGOZI wa Simba upo kwenye mazungumza ya kunasa saini na beki wa Namungo na timu ya taifa ya Burundi, Derrick Mukombozi kwaajili ya kuziba pengo la Henock Inonga ambaye anatajwa kutimka ndani ya kikosi hicho.

Simba wanapambana kunasa saini ya staa huyo wa Burundi ambaye ametupia mabao manne kwenye Ligi Kuu Bara iliyotamatika Mai 29 akiwa na Namungo na aliliambia gazeti hili anampango wa kuondoka msimu ukiisha.


KLABU ya Yanga Princess imeanza maandalizi mapema ya msimu ujao kwa kumfuata kiungo wa JKT Queens Amina Bilal ambaye mkataba wake unaisha mwishoni mwa msimu huu.

Nyota huyo aliwahi kuzitumukia timu za Kariakoo, Simba  na Yanga kabla ya kutua JKT, hivyo viongozi wa timu hiyo wameanza mazungumzo nae kujua namna gani watamrejesha kikosini hapo.

Yanga imeona haja ya kumrudisha kiungo huyo ambaye ana uwezo wa kucheza nafasi mbalimbali eneo la kati na hata kufunga mabao.


Kuna uwezekano mkubwa wa beki wa kushoto, Deusdedith Okoyo akajiunga na Pamba ya Mwanza iliyopanda daraja msimu huu. Kwa mara ya mwisho mchezaji huyo, alionekana na JKT Tanzania.

Mtu wa karibu na mchezaji huyo, alisema "Mazungumzo baina ya Okoyo na viongozi wa Pamba, yamefikia pazuri, kuna uwezekano msimu ujao, akawa sehemu ya kikosi hicho.


Maafande wa JKT Tanzania inasubiri mechi ya marudiano ya mtoano 'Play Off' dhidi ya Tabora Unite ili kujua hatma yake kusalia ligi kuu lakini tayari imeanza hesabu za usajili na jina la winga wa Kagera Sugar Richaldson Ng'odya.

Maafande hao ambao mechi ya kwanza ya Play Off walishinda kwa mabao 4-0 ugenini chini ya kocha Malale Hamsini wanamuhitaji Ng'odya aliyewahi kuwika na Mbeya City ili kuongeza nguvu kwenye kikosi hicho kwa msimu ujao.