Arsenal, Chelsea kwa vikosi hivi, itakuwaje!

LONDON, ENGLAND. KOCHA wa Chelsea, Mauricio Pochettino amepata pigo jingine ambalo mastaa wake watatu wanaweza kukosekana kwenye mchezo muhimu wa Ligi Kuu England dhidi ya Arsenal huko Emirates usiku wa leo Jumanne.

Wakati kikosi chake tayari kikiwakosa mastaa kama Reece James (paja), Wesley Fofana (goti), Lesley Ugochukwu (paja), Christopher Nkunku (paja), Romeo Lavia (paja), Robert Sanchez (mgonjwa) na Levi Colwill (kidole gumba), Pochettino amepata majeruhi wapya na kuzua wasiwasi akiwamo Cole Palmer, ambaye yupo kwenye hatihati ya kucheza mechi hiyo, huku Malo Gusto na Ben Chilwell wakifanyiwa uchunguzi.

Kikosi kinachotarajiwa cha Chelsea, ambacho kocha Pochettino anaweza kuanza nacho kwenye mechi hiyo ya ugenini ni Petrovic; Disasi, Chalobah, Badiashile, Cucurella; Fernandes, Caicedo; Sterling, Gallagher, Mudryk; Jackson kwenye fomesheni ya 4-2-3-1.

Wapinzani wao, Arsenal chini ya kocha Mikel Arteta hawatakuwa na mabadiliko makubwa sana kwenye kikosi chao kilichozoeleka; ambapo kwenye mfumo wa 4-3-3, kinatarajia kuwa hivi; Raya; White, Saliba, Gabriel, Zinchenko; Odegaard, Jorginho, Rice; Saka, Havertz, Martinelli. Kazi ipo.