Imefichuka, Xavi abadili uamuzi Liverpool

Muktasari:

  • Fundi huyu Mhispania mara kadhaa alikataa kubadilisha uamuzi wake wa kuondoka katika timu hiyo lakini sasa amekubali na hiyo ni baada ya kukutana na wajumbe wa bodu na rais wa timu hiyo.

IMEFICHUKA. Kocha wa Barcelona, Xavi anadaiwa kubadili uamuzi wake wa kuondoka katika timu hiyo mwisho wa msimu huu na badala yake anataka kubakia na kuendelea kuifundisha msimu ujao.

Fundi huyu Mhispania mara kadhaa alikataa kubadilisha uamuzi wake wa kuondoka katika timu hiyo lakini sasa amekubali na hiyo ni baada ya kukutana na wajumbe wa bodu na rais wa timu hiyo.

Rais wa Barca, Joan Laporta anadaiwa kuwa ndio amefanya kazi kubwa ya kumshawishi Xavi abaki jambo ambalo limechukua muda mrefu hadi kufanikiwa, kama ilivyoripotiwa na mwanahabari Fabrizio Romano.

Xavi aliisaidia Barcelona kuchukua taji la LaLiga msimu uliopita lakini msimu huu timu hiyo imekuwa ikipitia katika wakati mgumu.

Timu hii imeyumba kiuchumi hali inayosababisha kusiwe na usajili ambao Xavi aliupendekeza hadi ikasabisha timu isicheze anavyotaka yeye na mwisho akachukua uamuzi wa kutaka kuondoka.

Pia kumekuwa na ripoti zinazoeleza kwamba kuna mpasuko ndani ya timu hiyo ambapo wachezaji wamegawana makundi mbalimbali.

Katika taarifa yake ya kutangaza kuondoka Januari mwaka huu baada ya kichapo cha mabao 5-3 kutoka kwa Villarreal, Xavi alisema: "Nitaondoka hata kama tukishinda Ligi ya Mabingwa, nilishafanya uamuzi huu muda mrefu, watu wamekuwa wakiniambia kwamba naweza kuwa Sir Alex Ferguson wa Barcelona lakini hilo ni jambo gumu sana kulifanya katika timu hii, kuwa kocha wa Barca ni kazi ngumu sana."