Marcos Alonso anukia Atletico Madrid

Alonso Pict
Alonso Pict

Muktasari:

  • Alonso anaondoka baada ya kufanya vibaya msimu uliopita ambapo alicheza mechi nane tu za michuano yote kutokana na majeraha yaliyokuwa yanamwandama. Msimu wake wa kwanza alicheza mechi 45 za michuano yote na kufunga mabao matatu.

BEKI wa Barcelona ambaye ameachana na timu hiyo mwezi uliopita Marcos Alonso anatarajiwa kujiunga na Atletico Madrid katika dirisha hili kwa usajili huru.

Alonso anaondoka baada ya kufanya vibaya msimu uliopita ambapo alicheza mechi nane tu za michuano yote kutokana na majeraha yaliyokuwa yanamwandama. Msimu wake wa kwanza alicheza mechi 45 za michuano yote na kufunga mabao matatu.


BAYERN Munich bado inapambana kuhakikisha inamsajili beki wa Bayer Leverkusen, Jonathan Tah, 28, katika dirisha hili.

Tah ni miongoni mwa mastaa walioonyesha kiwango bora akiwa na Leverkusen kwa msimu uliopita ambapo aliisaidia timu hiyo kushinda taji la Bundesliga.

Mkataba wa sasa wa fundi huyu na Leverkusen unatarajiwa kumalizika mwaka 2025.


BADO mazungumzo yanaendelea baina ya mabosi wa San Diego ya Marekani na wale wa PSV Eindhoven kwa ajili ya usajili wa winga wa  PSV na Mexico, Hirving Lozano, 28, kutua San Diego katika dirisha hili.

San Diego inamtaka Lozano kutokana na kiwango bora alichoonyesha msimu uliopita ambapo alicheza mechi 33 za michuano yote na kufunga mabao sita.


CHELSEA imefikia hatua nzuri katika mazungumzo yake na Boca Juniors kwa ajili ya kuipata saini ya beki wa timu hiyo na Argentina, Aaron Anselmino, 21, katika dirisha hili.

Mabosi wa Chelsea wanataka kumsajili beki huyu kutokana na kiwango chake na umri wake mdogo kwani wamekuwa katika mpango kazi wa kuhakikisa wanasuka kikosi cha wachezaji vijana.


ARSENAL huenda ikakamilisha usajili wa beki wa pembeni wa  Fenerbanhce na Uturuki Ferdi Kadioglu, 24, ndani ya siku chache zijazo. Arsenal inataka kumsajili staa huyu baada ya kuvutiwa na kiwango bora alichoonyesha akiwa na kikosi cha Uturuki katika michuano ya Euro. Mkataba wa fundi huyu na Fenerbanhce unatarajiwa kumalizika mwaka 2026.


ARSENAL inataka kulipa zaidi ya Pauni 30 milioni kwenda Espanyol kwa ajili ya kuipata saini ya kipa wa timu hiyo, Joan Garcia, 23, katika dirisha hili. Kipa huyu anasajiliwa kwa ajili ya kutoa ushindani kwa Aaron Ramsdale ambaye msimu uliopita hakupata nafasi ya kutosha katika kikosi cha kwanza akitumika zaidi David Raya.


WEST Ham inaonekana kuwa na nafasi kubwa ya kuipata saini ya winga wa Hull City, Jaden Philogene, 22, ili kumsajili katika dirisha hili. Jaden ambaye pia anawindwa na Tottenham, amezivutia timu nyingi barani Ulaya kutokana na kiwango alichoonyesha msimu uliopita ambapo alicheza mechi 33 na kufunga mabao 12.