Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hii sasa sifa…! Harmonize ataka kupindua meza kwa Sugu, Jay Z

JESHI Pict

Muktasari:

  • Ni wazi mwimbaji huyo wa Konde Music amechagua eneo hilo kama sehemu ya kujipatia sifa kutoka mashabiki wake na hata kuweka rekodi ya kipekee katika tasnia ila kubwa zaidi ni kutaka kupindua meza kwa Mr. II Sugu na Jay Z.

STAA wa Bongofleva, Harmonize ametangaza kukamilika kwa albamu yake mpya ambayo inatarajiwa kuachiwa mwaka huu ikiwa ni ya sita ndani ya miaka sita mfululizo kitu ambacho hakuna msanii Bongo amewahi kufanya.

Ni wazi mwimbaji huyo wa Konde Music amechagua eneo hilo kama sehemu ya kujipatia sifa kutoka mashabiki wake na hata kuweka rekodi ya kipekee katika tasnia ila kubwa zaidi ni kutaka kupindua meza kwa Mr. II Sugu na Jay Z.

Akiwa bado chini ya WCB Wasafi ndipo aliachia EP yake ya kwanza, Afro Bongo (2019) yenye nyimbo nne alizowashirikisha mastaa wakubwa Afrika kama Diamond Platnumz, Yemi Alade, Mr. Eazi na Burna Boy.

Baada ya kuachana na lebo hiyo iliyomtoa kimuziki mwaka 2015, Harmonize ametoa albamu tano ambazo ni Afro East (2020), High School (2021), Made For Us (2022), Visit Bongo (2023) na Muziki wa Samia (2024).

Kwa ujumla albamu hizi zina nyimbo 80, hii inaonyesha ni kwa kiasi gani mwanamuziki huyo ana uwezo mkubwa wa kutunga, pia ana utajiri wa melodi zinazofanya nyimbo zake kupendwa na wengi.

JE 01

Albamu yake ‘Visit Bongo’ ilishinda Tuzo za Muziki Tanzania (TMA) kama Albamu Bora 2023 ikizibwaga ‘5’ ya Abigail Chams, ‘Swahili Kid’ ya D Voice, ‘Most People Want This’ ya Navy Kenzo na ‘Flowers III’ ya Rayvanny.

Ushindi huo ulimfanya kufikisha tuzo sita za TMA, tangu kurejeshwa kwa tuzo hizo msimu wa 2021, Harmonize ni miongoni wasanii walioshinda mara nyingi zaidi, wengine ni Zuchu (7), Alikiba (6) na Diamond (5) ambaye tangu 2010 kashinda mara 22.

Hata hivyo, hiyo ilikuwa mara ya kwanza kwa Harmonize kushinda kipengele cha Albamu Bora ya Mwaka TMA baada ya kuwania mara mbili mfululizo na kuondoka mikono mitupu!

Ikumbukwe albamu yake ‘High School’ iliwania TMA 2021 ikakosa, ilichuana na albamu nyingine kama ‘Ona’ ya Marco Chali, ‘Live At Sauti za Busara’ ya Wakazi, ‘Air Weusi’ ya Weusi na ‘Only One King’ ya Alikiba iliyoshinda. 

JE 02

Akarejea tena TMA 2022 na albamu yake ‘Made For Us’ ila akaangukia pua tena, awamu hii ilichuana na albamu kama ‘The Kid You Know’ ya Marioo, ‘Street Ties’ ya Conboi, ‘Romantic’ ya Kusah na ‘Love Sounds Different’ ya Barnaba iliyoshinda.

Kitendo cha kutangaza kutoa albamu ya sita ndani ya miaka sita mfululizo sio kwamba anataka kushinda tuzo pekee, bali kujizolea sifa tu na mwisho wa siku kuandika au kuweka rekodi yake katika Bongofleva. Kivipi?.

JE 06

Baada ya kuifikia rekodi ya Sugu aliyetoa albamu tano kwa miaka mitano mfululizo, sasa anataka kuivunja, Sugu mwenye albamu 10, albamu zake zilizofuatana ni Niite Mr II (1998), Nje ya Bongo (1999), Millennium (2000), Muziki na Maisha (2001) na Itikadi (2002).

JE 03

Kwa Afrika mwanamuziki aliyefanya hivyo hivi karibuni ni Burna Boy, mshindi wa Grammy kutokea Nigeria, albamu zake tano zilizofuatana ni Outside (2018), African Giant (2019), Twice as Tall (2020), Love, Damini (2022) na I Told Them... (2023).

Na rapa wa Marekani, Jay Z ana rekodi ya kutoa albamu nane kwa miaka minane mfululizo, albamu hizo ni Reasonable Doubt (1996), In My Lifetime, Vol. 1 (1997), Vol. 2... Hard Knock Life (1998), Vol. 3... Life and Times of S. Carter (1999).

Albamu nyingine ni The Dynasty: Roc La Familia (2000), The Blueprint (2001), The Blueprint 2: The Gift & The Curse (2002) na The Black Album (2003), kisha akatangaza kustaafu muziki na baadaye kuteuliwa kuwa Rais wa Def Jam Recordings.

JE 04

Ikiwa Harmonize ataendelea na mwendo huo, basi amebakiza miaka miwili ili kufikia rekodi ya Jay Z, mshindi wa Grammy 26 na rapa wa kwanza duniani kufikia hadhi ya ubilionea ambapo utajiri wake kwa sasa unakadiriwa kufikia Dola2.5 bilioni.

Ikumbukwe Harmonize si mwanamuziki pekee Bongo aliyetangaza kuachia albamu mwaka huu, kuna Lady Jaydee ambaye hapo Juni atatoa albamu yake ya 10 ambayo itaenda sambamba na kuadhimisha miaka yake 25 katika Bongofleva.

Lady Jaydee ambaye wimbo wake wa kwanza, Sema Unachotaka (2000) ulirekodiwa MJ Records, anatoa albamu 10 ndani ya miaka 25 huku Harmonize akitoa sita ndani ya miaka yake 10 katika Bongofleva tangu alipotoka na wimbo wake, Aiyola (2015).

JE 05

Hadi sasa baadhi ya wasanii wa Bongofleva wenye albamu nyingi ni Sugu (10), Lady Jaydee (9), Nikki Mbishi (8), Soggy Doggy (5), Juma Nature (5) Harmonize (5), Professor Jay (4), Mh. Temba (3), Fid Q (3), Diamond (3), Alikiba (3), Barnaba (3), Navy Kenzo (3) n.k.

Rapa Nikki Mbishi aliyevuma na ngoma yake, Play Boy (2010) chini ya M Lab (Music Laboratory), tangu mwaka 2011 hadi 2024 ametoa albamu nane ambapo alianza na Sauti ya Jogoo (2011) yenye nyimbo zake maarufu kama Kila Siku, Nyakati, Punchlines n.k.