Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwigizaji Carina azikwa makaburi ya Kisutu, Dar

Muktasari:

  • Carina alifariki dunia Aprili 15, 2025 nchini India alikoenda kupatiwa matibabu ya tumbo ambalo limemsumbua kwa zaidi ya miaka saba, huku akifanyiwa upasuaji mara 26.  

Aliyekuwa mwigizaji wa Filamu nchini marehemu Hawa Hussein (Carina), amezikwa leo Aprili 19,2025 katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.

Carina alifariki dunia Aprili 15, 2025 nchini India alikoenda kupatiwa matibabu ya tumbo ambalo limemsumbua kwa zaidi ya miaka saba, huku akifanyiwa upasuaji mara 26.  

Mwili wake uliwasili jana Aprili 18,2025 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na mara baada ya kuwasili ulisomewa dua kisha kupelekwa nyumbani kwao Magomeni Mapipa Mtaa wa Mvumi Dar es Salaam, ambapo ulilala hapo na mapema leo uliswaliwa katika msikiti wa Maamur, Upanga.

Februari 24, 2025, Carina alielekea India kupatiwa matibabu baada ya kukamilika kwa taratibu za safari na gharama ya matibabu Sh54 milioni ambazo zilitokana na michango ya serikali na tasisi mbalimbali.

Utakumbuka Carina alionekana kama Video Queen kwenye wimbo wa 'Oyoyo' wa kwake Bob Junior lakini pia alicheza kwenye tamthilia ya kwanza ya mwigizaji Jacob Stephen 'JB' ya mwaka 2017 hadi 2018 iliyoitwa 'Kiu ya Kisasi'.