Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rapcha, dogo sasa amekua!

Muktasari:

  • Kwa hiyo hata linapokuja suala la muziki msanii aliyezaliwa miaka ya efu mbili ni rahisi sana kuimba vitu ya anasa, lakini kwa Rapcha imekuwa tofauti. Wiki iliyopita aliachia albamu yake inayoitwa Don’t Take God’s Credit au Usichukue Sifa za Mungu. Nadiriki kusema kwamba mpaka kufikia leo hiyo ndiyo albamu bora kuliko zote zilizowahi kutoka mwaka huu.

RAPCHA amezaliwa Septemba 1999. Kwa hiyo kwa kulazimisha unaweza ukasema Rapcha ni mtoto wa ‘efu mbili’. Na wote tunajua kwa kawaida stori za madogo wa elfu mbili ni mambo ya mapenzi, bata, klabu, mademu, ngono, pombe, shisha, kutupia pamba kali na anasa zingine.

Kwa hiyo hata linapokuja suala la muziki msanii aliyezaliwa miaka ya efu mbili ni rahisi sana kuimba vitu ya anasa, lakini kwa Rapcha imekuwa tofauti. Wiki iliyopita aliachia albamu yake inayoitwa Don’t Take God’s Credit au Usichukue Sifa za Mungu. Nadiriki kusema kwamba mpaka kufikia leo hiyo ndiyo albamu bora kuliko zote zilizowahi kutoka mwaka huu.

Kwenye albamu hiyo Rapcha amejizeesha kwelikweli, ameimba mambo mazito utadhani sio mtoto wa efu mbili. Ameimba vitu ambavyo vitakufanya ukae chini usikilize, kisha usikilize tena halafu ukishaelewa utayatazama maisha yako na aidha kusema "Asante Mungu" kama sio kusema "Mungu nipe nguvu".

Albamu ina nyimbo 17; wakati nasikiliza nilikuwa naona kabisa Rapcha anaimba vitu ambavyo vilitakiwa kuimbwa na anko zake kina Fid au Joh sio mtoto wa efu mbili. Kwa mfano, sikiliza mistari hii kutoka kwenye wimbo wake wa Comfort Zone ambao unazungumzia madhara ya kuridhika kisha niambie inakuwaje mtoto wa efu mbili anaandika nyimbo zake namna hii:

Kupenda vitu rahisi inazaa uvivu,

Uvivu unazaa generation iliyojaa wivu,

Wivu unazaa ubinafsi na kurudishana nyuma,

Usilee mazoea mpaka yafanya uwe comfortable,

Kataa vitonga bro, I took from the bible,

Real man atakula kwa jasho na haipingwi hivyo,

Genesis chapter three, seventeen twenty four,

Tangu pale maisha hayajawahi kuwa comfortable..

Uandishi wa Rapcha kwenye albamu yake hii ya Usichukue Sifa za Mungu utakufanya ugundue kweli Mungu anatakiwa kusifiwa kwa kuumba wasanii wenye uwezo mkubwa hivi. Na sio suala la uandishi tu, kitu kingine ambacho nimekiona kwenye albamu hii ya Rapcha ni kuimba mambo mazito kwa ladha nzuri. Unajua, ni wasanii wengi wa hip hop wanajua kuimba vitu vya msingi, vitu ambavyo ni ujumbe ulioshiba. Ukisikiliza unatoka na kitu. Lakini mara nyingi changamoto huwa ni uwasilishaji wao.

Unakuta mtu anaimba vitu vya maana lakini uchanaji wake ni wa kizamani au anachana kiugumu sana. Lakini kwa Rapcha ni tofauti, uchanaji aliotumia humo ndani ukisema ubadilishe mistari na kuweka mistari fulani hivi ya kula gambe na stori za kumwaga mwanyuuu kwa mademu bado ngoma zitakuwa kali vilevile.

Nadhani kwenye suala la muziki wa hip hop Tanzania iko vizuri. Tuna madogo ambao tunaweza kuwategemea kwa miaka mingine kumi ijayo na Rapcha ameendelea kuthibitisha kwamba ni mmoja wa vijana hao kupitia albamu yake ya Usichukue Sifa za Mungu.