Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rich Mitindo: wanawake mniache nina mke

MITINDO Pict

Muktasari:

  • Rich Mitindo amesema, anatumiwa meseji nyingi za kinadada hasa katika mtandao wa kijamii wa Instagram, lakini kutokana na malezi aliyolelewa na wazazi wake anatakiwa awe na mwanamke mmoja tu ambaye tayari anaye.

MUME wa msanii wa filamu Jacqueline Wolper, Rich Mitindo, amewaomba msamaha wanawake wanaomtaka kimapenzi kupitia mitandao ya kijamii na kuwaambia kuwa hana utamaduni wa kuwa na wanawake wengi kutokana na malezi aliyolelewa na wazazi wake.

Rich Mitindo amesema, anatumiwa meseji nyingi za kinadada hasa katika mtandao wa kijamii wa Instagram, lakini kutokana na malezi aliyolelewa na wazazi wake anatakiwa awe na mwanamke mmoja tu ambaye tayari anaye.

“Mimi siwezi maisha ya kuhangaika na wanawake wengi, ndiyo maana nimefunga ndoa ili nitulie na mwanamke moja tu, sasa nawashangaa sana baadhi ya wanawake ambao wanafahamu kabisa kuwa nina mke lakini bado wananiletea vishawishi vya kunitongoza kiukweli nawaomba sana samahani waniache.”