Siri ya kinachombeba Rich Mavoko yafichuka!

Muktasari:

  • Mwimbaji huyo ambaye hivi karibuni ametangaza kuachia wimbo mpya ‘My G’, aliliambia Mwanaspoti kuwa, anafanya hivyo ili watu wasichoke kazi zake.

MKALI wa muziki wa kizazi kipya nchini, Rich Mavoko amesema siku zote anapenda kufanya vitu vinavyomzidi ndio sababu ya kufanya vizuri.

Mwimbaji huyo ambaye hivi karibuni ametangaza kuachia wimbo mpya ‘My G’, aliliambia Mwanaspoti kuwa, anafanya hivyo ili watu wasichoke kazi zake.

“Katika muziki wangu napenda kufanya vitu vinavyozidiana kila siku na sitamani watu wazoee ninachokifanya na hata ukisikiliza uandishi wangu unaona ni tofauti, napenda sana uandishi wangu nauheshimu sana,” alisema Mavoko.

Rich Mavoko, alisema kwa sasa akili yake ipo katika kuwaza vitu viwili muhimu, ambavyo ni jinsi ya kufanya nyimbo na jinsi ya kufanya promosheni ya nyimbo hizo ili ziwike ndio maana anakuwa kimya kwa muda na kuibuka.

Mkali huyo anatamba na ngoma kadhaa ikiwamo ‘Kokoro’, ‘Rudi’ na ‘Imebaki Stori na ni mmoja ya wasanii waliokuwa Lebo ya WCB kabla ya kujitoa kama ilivyokuwa kwa Harmonize na Rayvanny.