Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vaibu la Kautaka LilivyoIpaisha NYOTA YA Jaivah

KAUTAKA Pict

Muktasari:

  • Kutokana na maendeleo ya teknolojia yanafanya sasa kuwa rahisi muziki wa msanii kutoka nchi moja kusambaa hadi duniani na kufahamika kupitia kazi zake.

SANAA ya muziki kwa sasa inakua na imekuwa ajira kwa vijana wengi tofauti na hapo awali wasanii waliimba kwa kujitolea na kuburudisha zaidi watazamaji.

Kutokana na maendeleo ya teknolojia yanafanya sasa kuwa rahisi muziki wa msanii kutoka nchi moja kusambaa hadi duniani na kufahamika kupitia kazi zake.

Kwenye tasnia ya burudani wapo wasanii ambao ngoma moja tu huwafanya wajulikane zaidi kimataifa na kuwa na wafuasi wengi.

Mfano mzuri ni mwanadada Tyla wa Afrika Kusini ambaye hakuanza kazi muda mrefu, lakini baada ya kutoa wimbo wa ‘Water’ ulipenya duniani na kumfanya ashinde tuzo za Grammy.

Kwa Bongo pia iliwahi kutokea kwa wasanii kama Mr Nice na nyimbo zake kama ‘Kikulacho’, na ‘Kidali Po’, ambazo baada tu ya kutoka zikateka ukanda mzima wa Afrika Mashariki.

Zipo pia kama ‘Yule’ wa AY na ‘Nikusaidiaje’ wa Profesa Jay, ‘zeze’ wa TID na nyingine nyingi.

KAU 04

 Hilo bado linaendelea kujirudia kwani mwanamuziki wa kizazi kipya, Jaivah ambaye amefanya ngoma kibao lakini wimbo wake wa ‘Kautaka’ umeiteka zaidi Afrika ikiwamo Nigeria ulikovuma zaidi kuliko hata Bongo.


KILICHOMBEBA

Inawezekana sauti aliyotumia na biti za muziki vinafanana na ladha ya muziki wa Nigeria maarufu kama ‘AfroBeat’.

Wimbo huo alioutoa mwaka jana ukiingiza zaidi ya watazamaji milioni 1.5 Youtube na kufanya usikilizwe zaidi Nigeria kuliko Tanzania.

Mwaka jana ngoma hiyo iliingia kwenye Top 10 Streets Anthem ya MTV ambayo ni platform kubwa ya muziki wa Afrika.

Mbali na hiyo lakini mtandao wa Shazam uliitaja ‘Kautaka’ kama ngoma iliyoongoza namna moja Nigeria ikiwatupa mastaa wa nchini hiyo kama Rema Olamide na Omah Lay.

Kwa kuthibitisha ukubwa wa wimbo huo kuna video mbalimbali zilisambaa zikiwaonyesha mastaa wa Nigeria  kuwarusha wasanii wakubwa nchini Nigeria akiwemo Burna Boy, Mr Flavour, Tiwa Savage, Wizkid, Shallipo, Pocolee na wengine wengi.

KAU 01

Kitendo hicho kinaifanya ngoma ya msanii huyo kumtobolea mashavu ya madili mapya na kumpa mashabiki wengine nje ya Tanzania.


KAUTAKA YAMPA UMAARUFU

Kwa asilimia kubwa Kautaka ambao pia ni wimbo pendwa wa kocha wa zamani wa Yanga, Miguel Gamondi umemfanya Jaivah kumfungulia milango Nigeria ambako kumeonekana Bongo Fleva ni ngumu kutoboa huko.

Wimbo huo mwaka jana ulifanya vizuri kwenye chati za Nigeria na kupendwa na mashabiki wengi nchini humo ambao walivutiwa na sauti yake.

Baada ya wimbo huo kufanya vizuri Jaivah alifanya shoo na ziara baadhi ya sehemu nchini humo ambao alijizolea umaarufu mkubwa.

Hata alipofanyiwa mahojiano na Mwananchi Scoop, Jaivah alisema wimbo huo umempa mafanikio makubwa kimataifa.

KAU 02

“‘Kautaka’ inaendelea kufanya vizuri, mimi nipo Nigeria sasa. Baadhi ya wasanii walio-vibe na ngoma yangu nimepata nafasi ya kukutana nao. Lakini na vitu vingine vinaendelea, pale itapopaswa kuwekwa wazi basi itakuwa wazi,” anasema.

“Mwenyezi Mungu ajalie kama tutafanikiwa kufanya chochote basi kitaweza kutoka kwa sababu mimi kazi yangu ni kutoa burudani kwa watu.”

Kitendo cha kukutana na wakali hao huenda ikaleta mafanikio makubwa zaidi kwa Jaivah hasa kwenye kukuza mziki wake kimataifa.

Hilo halitaishia hapo kwani hizo ndio koneksheni zenyewe za kutoboa ingawa sio rahisi hasa kwa wasanii wakubwa ambao wana mambo mengi ya kibiashara za muziki.

KAU 03

Lakini kitendo cha kuzungumza japo kwa dakika chache na Davido, Wizkid ambao wana platform kubwa duniani itamsaidia kumwongezea mashabiki nje ya Tanzania.

Kwa sasa Jaivah nchini Nigeria ni miongoni mwa wasanii wanaofutiliwa hasa kazi zake zinapotoka na kuweka rekodi ya wimbo wake kufuatiliwa zaidi ugenini kuliko hata nyumbani kwao.