Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dili iliyokufa -2

Muktasari:

  •   Kabla ya kuiingia benki nilinunua mifuko miwili ya plasitiki ya kuwekea pesa. Nikiwa ndani ya benki hiyo nilikwenda katika kidirisha cha kutolea pesa, nikatoe ile hundi.

Mimi sikuwa na akaunti benki, wakinipa hundi itaniletea usumbufu.

“Nilikuwa na ombi, afisa wangu,” nikamwambia yule afisa baada ya kuandika jina langu.

“Matarajio yangu yalikuwa ni kupata fedha taslimu kwa sababu kama nilivyokuambia jana ninahitaji kwenda kununua mazao kwa ajili ya biashara na isitoshe kulikuwa na vitu nahitaji kununua hapa Dar es Salaam. Na pia nipate pesa ya nauli. Sasa ukinipa hundi utanikwamisha.”

“Kutoa hundi kwa malipo ndiyo utaratibu wetu. Sisi hapa hatuna pesa, isipokuwa naweza kukusaidia kukuandikia hundi ya wazi ili ukienda benki ulipwe pesa zako.”

“Itakuwa afadhali.”

“Lakini si kitu kizuri kushika mkononi kiasi kikubwa cha pesa kama hicho.”

“Ni kwa dharura. Nahitaji fedha za kulipa wakulima watakaoniuzia mazao yao. Vilevile nahitaji pesa za kununua vitu hapa Dar es Salaam pamoja na pesa ya nauli.”

“Sawa, lakini kuwa makini.”

  “Nitakuwa makini.”

SASA ENDELEA....


“SAWA lakini kuwa makini”

  “Nitakuwa makini”

  Tulipokubaliana na afisa huyo ndipo tukaenda katika ukumbi ilikoandaliwa sherehe ya kukabidhiwa hundi yangu. Hapo watu walikunywa soda na keki na kucheza mziki kidogo kisha nikakabidhiwa hile hundi. Baadaye nikapeana mikono na kuagana na wafanyakazi wa shirika hilo . Nikaondoka nikaenda katika benki niliyokuwa nimeelekezwa.

  Kabla ya kuiingia benki nilinunua mifuko miwili ya plasitiki ya kuwekea pesa. Nikiwa ndani ya benki hiyo nilikwenda katika kidirisha cha kutolea pesa, nikatoe ile hundi.

  Karani wa benki akaitazama ile hundi kisha akaniuliza.  “Ni  ya nani?”

  Nikamjibu.  “Ni yangu”

  “Mbona hukuweka sahihi?” akaniuliza huku akinirudishia . “Weka sahihi yako huku nyuma”

  Wakati akiniambia hivyo nilishtuka nilipomuona Dastani lazaro akipita nyuma yangu huku ameikodolea macho ile hundi. Nikajifanya sikumuona.

  Nikaweka sahihi yangu nyuma ya ile hundi kisha nikampa yule karani wa benki.

Karani wa benki akanipatia bunda la shilingi milioni kumi nikazitia kwenye mfuko wangu wa plastiki. Baada ya hapo nikatoka na kuzunguka kwenye maduka. Nilinunua kila kitu nilichohitaji. Nakumbuka nilijaza mabegi mawili ya vitu vyangu.

Nikarudi kule hoteli. Nilipoingia chumbani, kwanza niliweka pesa zangi chini ya godoro. Nikavitoa vile vitu nilivyonunua na kuviweka juu ya kitanda. Nilikuwa nimenunua nguo zangu na vitu vingine. Pia nilinunua kamera moja na vitu vingine vidogo vidogo.

Baada ya kuvikagua vitu hivyo niliwasha ile redio ndogo, ikawa inapiga miziki. Nikaaza kujaribu zile nguo nilizonunua kisha nikajiangalia kwenye kioo cha kabati. Kwa kweli nilipendeza sana .

Nguo nilizozijaribu mwisho skuzivua tena. Nikapanga vitu vyangu kwa umakini  kwenye lile sanduku na yale mabegi. Nilipomaliza niliketi na kuanza kupanga safari ya kurudi Muheza.

Wakati ninawaza nikasikia tangazo kwenye redio kuwa Bendi ya Juwata itapiga mziki siku ile katika ukumbi mmoja uliopo Kinondoni.

Kusema kweli nilikuwa mbovu sana wa miziki na nilikuwa nikiipenda sana bendi ya Juwata  enzi hizo lakini sikuwahi kuhudhuria  kwenye onesho lao lolote mbali ya kuwasikia kwenye redio.

Nikaona niahirishe safari yangu ya kurudi Muheza ili niende nikawaone vijana hao wa Juwata,   halafu kesho yake niondoke asubuhi

Nilipofikia uamuzi  huo nilibaki mle chumbani nikisikiliza redio hadi saa moja usiku nilipokwenda kuoga. Nilipomaliza nilivaa nguo zangu miongoni mwa zile nguo nilizonunua. Nikavaa viatu vipya na saa yangu mipya.

  Mfukoni nilitia shilingi laki tatu nikatoka. Nilikwenda kula chakula kisha nikakodi teksi na kumwambia dereva anipeleke Kinondoni

  Wakati  teksi ikielekea Kinondoni  ulikokuwa ukumbi huo, nilikuwa nikilitazama jiji kwenye dirisha. Lilikuwa liking’ara kutokana na taa zilizokuwa zikiwaka kwenye majumba na zile zilizokuwa kandoni mwa barabara.

  Teksi ilinifikisha Kinondoni na kusimama mbele ya ukumbi wa vijana ambapo bendi ya Juwata  ingeporomosha muziki hadi saa kumi alfajiri.

  Niliposhuka kwenye teksi nilikwenda kujiunga katika msururu wa wakata tikiti. Kwa vile msururu ulikuwa mrefu ilinichukua karibu dakika tatu kufika katika  kidirisha cha kukatia tikiti. Nilipokata tikiti yangu niliingia ndani ya ukumbi huo uliokuwa unaanza kujaa watu.

  Nilitafuta meza  iliyokuwa tupu  nikaketi kuelekea upande uliokuwa na jukwaa. Muhudumu aliponifata kuniuliza nataka nini, nilimwagiza bia baridi. Nilipoletewa bia niliyoagiza nilianza kunywa taratibu .

  Mpaka muziki unaanza nilikuwa nimekunywa chupa tatu za bia ambazo nilizinywa taratibu. Wakati ninamalizia chupa ya tatu nikamuona mwanaume na mwanamke wakija kwenye meza niliyokuwa nimekaa.

Sikuweza kuwatambua mpaka walipoketi.

  Mwanaume alikuwa ni rafiki yanga Dastani Lazaro. Nilijisikia furaha kupata mwenyeji katika ukumbi huo, nikamlaki.

  “Oh? Dastani ni wewe?”

  “Ni  mimi mgosi. Habari za tangu jana?” Dastani akaniuliza.

  “Nzuri mgosi. Nimefurahi tumekutana tena“

  “Huyu ni shemeji yako mgosi, anaitwa Vicky »

Dastani akanionyesha yule msichana aliyekuwa naye ambaye kutokana na mavazi yake alionekana kama changudoa.

  “Nimefurahi kumfahamu. Karibu shemeji.”

  Dastani akaendelea kututambulisha.

  “Na huyu bwana ni rafiki yangu wa nyumbani kabisa, yaani ni kama ndugu. Anaitwa Wakwetu.” Dastani alinionyesha mimi.

  “Okay shemeji, habari za siku ?” Msichana akanisalimia.

  “Nzuri tu. Mtakunywa nini?”

  Msichana akamtaza Dastan.

  “Acha tuagize bia” Dastani alisema na kumpungia muhudumu. Muhudumu alipofika alimuagizia bia mbili na mimi nikaagiza bia ya nne.

  Bia hizo zilipoletwa tuliendelea kunywa huku tukizungumza.

  “Mgosi mimi nina mwenzangu lakini naona wewe upo peke yako” Dastani aliniambia.

  “Si unajua mgosi….. ugeni”

  “Usijali mgosi, yuko shemeji yangu humu ndani . Utakuwa naye”

  “Nitafurahi mgosi”

  Chupa nne za bia tayari zilikwisha nilewesha. Nilikuwa sizingatii tena yale tuliyokuwa tunazungumza. Nakumbuka yule msichana aliondoka nikadhani anakwenda kujisaidia lakini badaye  kidogo alikuja na msichana mwingine aliyejiunga na sisi.

  “Shemeji kutana na mdogo wangu  akuchangamshe “ Vicky akaniambia. Nikamwagizia bia yule msichana.

  Dastani na Bibi yake waliondoka kwenda kucheza wakaniacha mimi na yule msichana mwingine. “Kumbe unaitwa nani?” nikamuliza msichana huyo.

  “Ninaitwa Suzy. Wewe je?”

  “Mimi ninaitwa Wakwetu.”

  “Unaishi wapi?”

“Ninaishi Buguruni na wewe unaishi wapi?”

  “Kwa kweli nipo hotelini. Nimekuja Dar mara moja tu”

  “Unatokea wapi?”

  “Natokea Muheza mkoani Tanga”

Tukaendelea kuzungumza hadi muziki ukamalizika. Nikaondoka na yule msichana. Tukiwa kwenye teksi aliniuliza ninaishi hoteli gani.

Nilipomtajia hoteli ninayoishi akanambia. “Hoteli chafu sana ile na haina hadhi. Mimi siwezi kukaa kwenye hoteli ile. Hebu tuhame twende hoteli nyingine.”

 Kwa sababu ya upumbavu, maneno yake yakaniingia. Tulipofika hapo hoteli na kumwambia anayehusika na kutoa vyumba kuwa ninaondoka usiku ule akanisihi sana nisiondoke usiku ule lakini sikumsikiliza.

Nikaingia chumbani na kumpa suzi sanduku langu akalipakie kwenye teski. Mimi nikawa ninatoa zile pesa kwenye godoro na kuzitia kwenye mfuko wa plastiki

 Suzi aliporudi tena nilimpa yale mabegi akatoka nayo. Mimi nilibeba ile redio kubwa pamoja na mfuko wa pesa nikatoka

 Karani wa vyumba akanidaka kwenye mlango na kuniambia”Hebu sikiliza bwana. unajuwa wewe umelewa na huu ni usiku kwa nini usisubiri asubuhi ndio uondoke?”

Kabla sijajibu kitu suzi akaingilia kati.

“Kwani wewe shida yako ni nini? kama mteja hataki kukaa kwa nini unamlazimisha?”

“So kama ninamlazimisha. ninajaribu kumshauri kwa sababu za kiusalama” karani akaniambia

Suzi akanishika  mkono na kunikokota

“Twende zetu bwana asitunzinguwe”

Nikamfata Suzi kama mbwa aliyekuwa akijipeleka midomoni mwa chatu: Jamaa alikuwa akiniangalia kwa nyuma. bila shaka alikuwa akinisikitikia

“Hachana na sisi.” Nikaenda huku nikiropoka

“Shauri yako bwana,” karani huyo akaniambia

Tulitoka nje ya hoteli tukajipakia kwenye ile teski pamoja na mizigo yetu.

Tukaondoka.