Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dili iliyokufa - 6

HADITHI Pict

ILIPOISHIA

“Subiri,” akaniambia huku akishuka. Alikwenda kwenye mlango ambao ulikuwa wazi, akapiga hodi. Hakukuwa na jibu lakini aliingia hivyo hivyo. Nilipomuona anaingia na mimi nilifungua mlango wa teksi nikashuka na kumfuata. Niliingia humo ndani. Nyumba ilikuwa kimya. Dereva huyo alikwenda hadi mlango wa uani akatoka uani, kitu kilichonidhihirishia kuwa alikuwa mwenyeji.

Endelea....

Nilipiga hatua za haraka haraka na mimi nikafika uani. Nilipotupa macho nilimuona akiingia kwenye chumba kimoja miongoni mwa nyumba tatu zilizokuwa uani.

SASA ENDELEA...


Kwa ile hamaki yangu kuwa humo ndimo anamoishi Dastan, niliingia bila kubisha hodi.

Nilimkuta msichana ameketi kwenye kitanda. Nilipomwangalia vizuri niligundua kuwa alikuwa yule msichana niliyekuwa naye usiku. Alikuwa akijaribu kuifungua ile redio yangu kubwa iliyokuwa juu ya kitanda. Kando ya kitanda palikuwa na meza. Vitu vyangu vilikuwa vimepangwa juu ya meza kama vile vinauzwa.

Yule msichana akageuka na kunitazama. Uso wake uliingiwa na shaka aliponiona. Sikujua kama alinitambua au la.

“Si nimekuambia unisubiri ndani ya teksi?” dereva wa teksi akaniambia.

“Kwani umekuja naye wewe?” yule msichana akamuuliza.

“Alipatana na Dastan amuuzie redio.”

Msichana huyo akanitazama tena. Alikuwa kama anajiuliza ndiye mimi waliyenikwapua usiku au siye.

“Yuko wapi Dastan?” dereva wa teksi akauliza.

“Dastan anaoga. Kama amepatana naye, amsubiri,” msichana akajibu, lakini uso wake ulikuwa bado na shaka.

“Redio yenyewe ndiyo hii,” dereva wa teksi akaniambia.

“Nimeiona. Anaiuza kiasi gani?”

“Msubiri Dastan aje, atakuambia bei yake. Bado ni mpya kabisa.”

“Nimeiona ni mpya. Itanifaa sana.”

“Si umekuja na pesa?”

“Ndiyo, pesa zipo. Hata akitaka kwa laki moja nitanunua.”

“Basi kaa hapo kwenye kiti tumsubiri.”

Palikuwa na kiti karibu na mlango, nikaketi. Yule msichana alikuwa akiendelea kunitazama kwa wasiwasi. Hakuonesha kuwa na furaha hata chembe.

Wakati ninaketi, mlango ulifunguliwa, Dastan akaingia. Alikuwa amejifunga taulo kiunoni na mkononi alishika mswaki na kifaa cha kuhifadhia sabuni.

Alinidanganya kuwa ana nyumba yake Buguruni, kumbe anaishi katika chumba cha uani kisicho na hadhi yoyote, nilijiwazia kimoyomoyo.

Dastan aliponiona alishtuka.

“Vipi?” akauliza huku akijizuia sauti yake isionyeshe hofu aliyoipata.

“Jamaa amekuja, anataka ile redio. Amekuja na pesa,” dereva wa teksi akamwambia bila kujua kilichokuwa kwenye hisia za mwenzake.

Badala ya kujibu, Dastan alibaki ameduwaa.

Hapo hapo nilinyanyuka kwenye kiti. Nikamvamia Dastan na kumtia kabali. Nilihakikisha nimemdhibiti sawasawa.

“Wewe Dastan, ulinifanya mimi jogoo la shamba, nisiwiki mjini. Lakini leo nitawika. Nataka pesa zangu na vitu vyangu mlivyoniibia!” nikamwambia Dastan kwa sauti kavu. Wakati huo nilikuwa nimeshapandisha mizuka ya kwetu.

“Hebu niachie...” Dastan alisema huku akijaribu kujikukurua ili autoe mkono wangu, lakini hakuweza. Nikaendelea kumkaba koo.

“Utaniua...” Dastan alilalamika sauti yake ikiwa haitoki. Mdomo wake ulikuwa wazi na ulimi umemtoka.

“Nitakuua kweli. Nataka pesa zangu!”

“Hebu ngoja kwanza. Kwani wewe ni nani?” dereva wa teksi alisema akijaribu kunishika.

“Mimi nilijua tu kuwa kutazuka jambo!” msichana naye akasema huku akinyanyuka.

“Tafadhali usinishike!” nilimuonya dereva wa teksi.

“Muondoe, atamuua mwenzake,” msichana akasema.

Nilipomwona dereva wa teksi anataka kunishika, niliburuzana na Dastan kuelekea ukutani. Dereva wa teksi aliponifuata, nilimsukumia teke tumboni. Teke hilo lilimpeleka kwenye mlango, akaung’oa mlango na kuanguka nao uani.

Msichana alipoona vita vimeanza, aliinama chini ya mvungu wa kitanda akatoa mfuko mweusi ambao ulikuwa umejaa kitu. Akaukunjakunja na kuharakisha kutoka.

Nilishuku kwamba ule mfuko ndiyo uliokuwa na pesa walizoniibia. Nikamuacha Dastan na kumvamia yule msichana. Alining’ata mkono ili nimuachie, nikampiga ngumi iliyomtupa kwenye kitanda. Mfuko alikuwa bado anao. Alijaribu kuinuka nikamfuata. Nilimpiga ngumi nyingine kali zaidi. Akauacha mfuko na kulala kitandani.

Wakati nataka kuuchukua mfuko huo, Dastan alinishika kwa nyuma. Nikampiga kwa kiwiko cha mkono wangu wa kulia. Kiwiko kilimpata kwenye shavu, kikamrudisha nyuma. Nikageuka. Sikumngoja ajiweke sawa, nilimpiga ngumi kisha nikaokota stuli na kumpiga nayo kichwani.

Dastan alianguka chini, hakunyanyuka tena. Nikauchukua ule mfuko nikauangalia ndani. Kulikuwa na noti nyekundu tupu. Nikaukunjakunja na kuuweka kwapani.

Ghafla nikaona watu wanaingia humo chumbani. Nikahisi walikuwa wapangaji wengine wa ile nyumba.

“Kuna nini jamani, mbona mnapigana na kung’oa milango?” mpangaji mmoja akaniuliza.

Nikawaeleza. Wale watu waliposikiliza maelezo yangu walishituka. Mzee mmoja akaniambia:

“Sasa usitoke humu ndani mpaka tuite polisi.”

“Sawa,” nikamjibu.

Mle chumbani waliingia watu watatu wakawa kama walioniweka chini ya ulinzi. Huku uani kulikuwa na watu wengine ambao sikujua walikuwa wangapi.

Kulikuwa na mpangaji mmoja miongoni mwa wale waliokuwa uani aliyepiga simu kuita polisi.

Sikuwa na wasiwasi sana. Kwa vile pesa na vitu vyangu nimeshavipata, nilijua kila kitu kingekwenda sawa. Ripoti ya kuibiwa pesa zangu walikuwa nayo polisi, hivyo wakifika nitawaeleza ukweli na kuwaonesha watu walionifanyia ushenzi huo.

Sikufikiri kama nitakuwa na kesi ya kukutwa na madawa ya kulevya kwani nilikwisha eleza kwamba kete hiyo niliwekewa mfukoni na akina Dastan ili nionekane ni mlevi wa unga.

Pengine walidhani ningekamatwa na kwenda kufungwa na hivyo nisingeweza kuwatafuta.

Pia sikufikiri kuwa polisi hao wangeweza kunifungulia kesi kwa sababu ya kuwatoroka kwani tangu hapo sikuwa na kosa. Na kuwatoroka kwangu ndiko kulikosababisha wezi wangu wapatikane. Kwa hiyo nilikuwa nimeisaidia polisi.

Nikamwona Dastan aliyekuwa amepoteza fahamu akianza kuzinduka. Aliponyanyuka akaambiwa akae awasubiri polisi.

“Nani ameita polisi?” akauliza kwa kutaharuki.

Wapangaji wenzake wakamweleza juu ya madai yangu ya kuibiwa pesa na vitu vyangu. Hapo hapo Dastan akanikana.

“Huyu ni mwizi!” akasema. “Mimi simtambui. Msisikilize maneno yake. Yaani alitakiwa apigwe kabla hata ya polisi hao kufika.”

“Hapana. Kama ni mwizi tayari tumeshamdhibiti. Acha tuwasubiri polisi,” mzee mmoja akamwambia.

Lakini Dastan hakukubali. Aliendelea kunituhumu na kudai kuwa pesa nilizochukua zilikuwa zake.

Kama si zile pesa nilizokuwa nimezishika, ningenyanyuka na kumpa mkong’oto, lakini nilihofia pesa hizo zingeweza kuchukuliwa na watu wengine na pengine nisingezipata tena, hivyo niliona ninyamaze.

Mara moja polisi wakafika. Mmoja wa polisi hao alikuwa katika kundi la wale polisi walionikamata asubuhi. Aliponiona tu alinitambua.

“Wewe ulitutoroka asubuhi,” akaniambia.

“Ni kweli niliwatoroka lakini lengo lilikuwa ni kuwatafuta wezi wangu. Sasa nimeshawapata.”

“Wako wapi?”

Nikawaonesha Dastan na yule msichana aliyekuwa ameketi kitandani.

Polisi hao walipomwona Dastan wakashituka.

“Wewe bwana tulikuwa tunakutafuta sana. Tuna kesi nyingi na wewe. Kumbe jina lako halisi ni Dastan,” mmoja wa polisi hao akamwambia Dastan.

Nikashukuru kuona kuwa hata polisi walikuwa wakimfahamu.

Polisi aliyekuwa akinitambua aliwaeleza wenzake kisa kilichokuwa kimenitokea asubuhi mpaka nilivyowatoroka kwenye hoteli.

“Sasa uliwezaje kuwapata?” polisi huyo akaniuliza.

Nikawaeleza nilivyofikishwa hapo na dereva wa teksi namba 1000 niliyoikuta pembeni mwa Barabara ya Lumumba.

Baada ya maelezo yangu, polisi hao walimkamata Dastan na yule msichana wakawapakia kwenye gari la polisi. Vile vitu vyote walivyoniibia vikachukuliwa. Mimi nilibaki na mfuko wangu wa pesa. Nikaambiwa niingie kwenye gari.

Kwanza tulikwenda kule hotelini. Karani wa hoteli hiyo alipoulizwa kama alikuwa anamtambua Dastan alisema:

“Kwanza huyu msichana ndiye aliyekuwa na huyu mlalamikaji jana usiku. Na huyu jamaa, kama sikosei, alikuwa ndani ya gari. Alikaa siti ya nyuma.”

“Mimi uliniona?” Dastan alijitia kuuliza kwa mshangao.