Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mastraika Mashujaa haitokei kwa bahati mbaya

MASHUJAA Pict

Muktasari:

  • Msimu uliopita, Kibaya alifunga mabao sita, Bwenzi alipachika matano, Salum Kihimbwa alifumania nyavu mara nne, Crispin Ngushi alifunga matatu kama ilivyo kwa Seif Karihe na David Uromi.

INASHANGAZA kuona Mashujaa FC ni miongoni mwa timu zilizofunga idadi ndogo ya mabao katika Ligi Kuu Bara msimu huu hadi sasa.

Katika kupitia msimamo wa ligi hapa kijiweni, tumeona Maafande hao hadi sasa wamefunga mabao tisa tu katika mechi 18 za Ligi Kuu ambazo wameshazicheza.

Hii maana yake ni Mashujaa FC wanafunga bao moja kila baada ya mechi mbili na kwa wale wenzangu na mimi ambao somo la hisabati kidogo halikuwapiga chenga wanaweza kukubaliana na kijiwe kwa kukadiria, Mashujaa haijafunga bao kwa angalau nusu ya mechi ilizocheza msimu huu.

Jambo la kushtua zaidi ni mfungaji wao bora hadi sasa ni Mundhir Vuai ambaye amefunga mabao mawili tu huku mengine saba yakifungwa na Hassan Haji, Abdul Bakari, Japhary Kibaya, Baraka Mtuwi, Nyenyezi Shaban, Idrisa Stambuli na Selemani Bwenzi.

Hata hivyo, kwa tathmini ya kiandamizi hapa katika kijiwe, tumebaini kuna namna benchi la ufundi la Mashujaa linastahili kunyooshewa kidole kwa hicho kinachotokea kwa timu kuwa na ubutu wa ushambuliaji.

Inaonekana kama makocha ambao wamepata fursa ya kuifundisha Mashujaa msimu huu wameshindwa kuandaa mikakati mizuri ya kimbinu kwa ajili ya kupata kilicho bora kutoka kwa kundi kubwa la washambuliaji waliopo katika timu hiyo.

Labda staili ya kiuchezaji ya timu haiko sawa ama makocha wameshindwa kulinda makali ya washambuliaji wao msimu jambo linalofanya wachezaji hao washuke viwango vyao vya kiushambuliaji msimu huu.

Msimu uliopita, Kibaya alifunga mabao sita, Bwenzi alipachika matano, Salum Kihimbwa alifumania nyavu mara nne, Crispin Ngushi alifunga matatu kama ilivyo kwa Seif Karihe na David Uromi.

Haiwezekani eti wote hao msimu unaofuata hadi mechi ya 18 kiujumla wakafunga mabao mawili tu lazima kuna shida upande wa benchi la ufundi.