Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mossi Nduwumwe karibu Kariakoo

MOSI Pict

Muktasari:

  • Kama hilo likitimia, haitokuwa jambo la kushangaza hapa kijiweni kwani Singida Black Stars haina baya kwa Yanga pindi inapomhitaji mchezaji wao awe staa au hata awe na kiwango cha kawaida.

TAARIFA ambazo kijiwe kimezisoma zinaripoti Mfungaji Bora wa Ligi Kuu msimu wa 2025/2026, Mossi Nduwumwe anajiandaa kuishi Dar es Salaam msimu ujao.

Tetesi zinadai mwamba huyo kutoka Burundi ataitumikia Yanga katika msimu wa 2026/2027 akichukua nafasi ya mchezaji mmoja wa kigeni.

Kama hilo likitimia, haitokuwa jambo la kushangaza hapa kijiweni kwani Singida Black Stars haina baya kwa Yanga pindi inapomhitaji mchezaji wao awe staa au hata awe na kiwango cha kawaida.

Kuna zaidi ya wachezaji 10 ambao wamehama kwa kubadilishana katika timu hizo mbili na hapana shaka hilo linachangiwa na mahusiano mazuri ambayo pande hizo zimekuwa nayo kwa muda mrefu.

Kijiwe kwanza kinampongeza Mossi Nduwumwe kwa kuibuka Mfungaji Bora huku akiwa amesajiliwa katika dirisha dogo la usajili kwani amefanya kazi kubwa sana ndani ya muda mfupi.

Mabao 17 aliyofunga Nduwumwe ndani ya miezi sita, kuna wachezaji wengi wa nafasi ya ushambuliaji hapa nchini wameshindwa kuyafunga kwa zaidi ya misimu mitano.

Yaani baadhi ukijumlisha mabao ambayo kila mmoja amefunga katika misimu mitano, hayafiki 17 yaliyofungwa na Nduwumwe ndani ya miezi michache aliyocheza katika msimu uliomalizika.

Hata hivyo kama anakuja Kariakoo, Nduwumwe anapaswa kujipanga vilivyo na kuongeza umakini kwani anaenda katika timu ambayo ina presha na mahitaji makubwa kuliko anayotoka.

Uvumilivu na utulivu ambao anaupata Singida Black Stars asitegemee ataupata kwa miamba ya Kariakoo.