Prime
Yanga ilivyozipiga bao Simba, Azam
MASHABIKI wa Yanga hawaridhishwi na kiwango cha kikosi hicho kwa sasa baada ya kutoka sare mechi tatu mfululizo za Ligi Kuu Bara, lakini licha ya yote hayo mabingwa hao watetezi wamezipiga bao Simba na Azam FC.
Sare hizo tatu mfululizo zilizoibua maneno ya kutorishwa kwa mashabiki wa timu hiyo zilianza Machi 15, 2026 kwa suluhu dhidi ya Azam kisha Machi 18, 2026 kwa TRA United na ile ya Machi 21, 2026 ya kufungana bao 1-1 na Mtibwa Sugar.
Wakati Ligi Kuu ikisimama kwa sasa ili kupisha kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), Yanga ndio timu pekee iliyokusanya pointi nyingi zaidi katika mechi za nyumbani na genini msimu huu ikizipiga bao Simba na Azam.
Kupitia makala hii, Mwanaspoti linakuletea uchambuzi wa timu za Yanga, Simba na Azam, na kile zilichovuna msimu huu katika mechi za Ligi Kuu Bara zilizozicheza nyumbani na ugenini.
YANGA
Licha ya kutoka sare mechi tatu mfululizo, ila, Yanga inashikilia rekodi nzuri ya kutopoteza pambano la Ligi Kuu Bara, tangu mara ya mwisho kwa kikosi hicho, kilipochapwa na TRA United zamani Tabora United kwa mabao 3-1, Novemba 7, 2024.
Tangu Novemba 7, 2024, Yanga imecheza mechi 36 za Ligi Kuu bila ya kupoteza, ambapo kati ya hizo kikosi hicho cha mitaa ya Twiga na Jangwani, kimeshinda 30 na kutoka sare sita, kikifunga mabao 101 na kuruhusu nyavu zake kutikiswa mara tisa.
Kwa msimu huu wa 2025-2026, Yanga imecheza mechi 16, za Ligi Kuu Bara, ambapo kati ya hizo nane ni za nyumbani na nane nyingine ni za ugenini, ambazo zimeifanya kikosi hicho kuendelea kubakia kileleni mwa msimamo kwa kukusanya pointi 38.
Katika mechi nane za nyumbani, Yanga imeshinda saba na kutoka sare mmoja tu, ikikusanya jumla ya pointi zake 22, ambapo safu ya ushambuliaji ya kikosi hicho imefunga mabao 25, huku ikiruhusu pia nyavu zake kutikiswa mabao mawili hadi sasa.
Kwa upande wa mechi nane ilizocheza ugenini, Yanga imeshinda nne na kutoka pia sare nne, ikikusanya jumla ya pointi 16, ambapo safu yake ya ushambuliaji ya kikosi hicho imefunga mabao saba, huku ikiruhusu nyavu zake kutikiswa mara moja tu.
MECHI ZA YANGA NYUMBANI
(1)-Yanga 3-0 Pamba Jiji
(2)-Yanga 2-0 Mtibwa Sugar
(3)-Yanga 4-1 KMC FC
(4)-Yanga 2-0 Fountain Gate
(5)-Yanga 6-0 Mashujaa FC
(6)-Yanga 3-1 Dodoma Jiji
(7)-Yanga 5-0 JKT TZ
(8)-Yanga 0-0 Simba
JUMLA YA MECHI-8
USHINDI-7
SARE-1
MABAO YA KUFUNGA-25
MABAO YA KUFUNGWA-2
POINTI-22
MECHI ZA YANGA UGENINI
(1)-Mbeya City 0-0 Yanga
(2)-Coastal Union 0-1 Yanga
(3)-Namungo FC 0-1 Yanga
(4)-Singida BS 0-3 Yanga
(5)-TZ Prisons 0-1 Yanga
(6)-Azam FC 0-0 Yanga
(7)-TRA United 0-0 Yanga
(8)-Mtibwa Sugar 1-1 Yanga
JUMLA YA MECHI-8
USHINDI-4
SARE-4
MABAO YA KUFUNGA-7
MABAO YA KUFUNGWA-1
POINTI-16
SIMBA
Simba inayosaka taji la Ligi Kuu Bara msimu huu baada ya kulikosa kwa misimu minne mfululizo na kushuhudia likibebwa na watani zao wa jadi Yanga, kwa sasa kikosi hicho kinachonolewa na Kocha, Steve Barker, kiko nafasi ya pili na pointi 31.
Timu hiyo imecheza mechi 14, za Ligi Kuu kwa msimu huu wa 2025-2026, ambapo kati ya hizo saba ni ya nyumbani na nyingine saba ni ya ugenini, ikiendelea kuleta ushindani mkali katika vita ya kuwania ubingwa dhidi ya mabingwa watetezi, Yanga.
Katika mechi saba ilizocheza nyumbani, Simba imeshinda mitano, ikitoka sare mmoja na kuchapwa pia mmoja, ikiwa na pointi 16, huku safu yake ya ushambuliaji ya kikosi hicho ikifunga mabao 15, huku ikiruhusu nyavu zake kutikiswa mara tatu tu.
Kwa upande wa mechi saba za ugenini ilizocheza Simba kwa msimu huu, imeshinda nne na kutoka sare tatu, sawa na kukusanya jumla ya pointi 15, ambapo safu ya ushambuliaji imefunga mabao tisa, huku ikiruhusu nyavu zake kutikiswa mara tatu tu.
MECHI ZA SIMBA NYUMBANI
(1)-Simba 2-0
Mashujaa FC
(2)-Simba 1-1 Mtibwa (3)-Simba 0-2 Azam FC
(4)-Simba 3-0 Mbeya City
(5)-Simba 3-0
Namungo FC
(6)-Simba 3-0 Fountain Gate
(7)-Simba 3-0 TRA United
JUMLA YA MECHI-7
USHINDI-5
SARE-1
KUPOTEZA-1
MABAO YA KUFUNGA-15
MABAO YA KUFUNGWA-3
POINTI-16
MECHI ZA SIMBA UGENINI
(1)-Pamba Jiji 1-1 Simba
(2)-Singida BS 1-2 Simba
(3)-Yanga 0-0 Simba
(4)-Dodoma Jiji 0-0 Simba
(5)-TZ Prisons 0-2 Simba
(6)-KMC FC 0-2 Simba
(7)-JKT TZ 1-2 Simba
JUMLA YA MECHI-7
USHINDI-4
SARE-3
MABAO YA KUFUNGA-9
MABAO YA KUFUNGWA-3
POINTI-15
AZAM FC
Timu hii inayonolewa na kocha mzoefu, Mkongomani Florent Ibenge, inasaka taji la kwanza la Ligi Kuu Bara, tangu mara ya mwisho kikosi hicho kilipotwaa msimu wa 2013-2014, ambapo msimu huu inashika nafasi ya tatu katika msimamo na pointi 29.
Katika mechi 15, iliyocheza Azam, saba ni ya nyumbani, ambapo timu hiyo imeshinda nne tu na kutoka sare tatu, ikikusanya pointi 15, huku safu ya ushambuliaji ikifunga mabao 10, wakati eneo la kujilinda hadi sasa halijaruhusu bao lolote lile.
Kwa mechi za ugenini msimu huu, Azam imecheza minane, ikishinda mitatu na kutoka sare mitano, sawa na kukusanya pointi 14, ambapo kiujumla safu ya ushambuliaji ya timu hiyo imefunga mabao 11, huku ikiruhusu nyavu zake kutikiswa mara nne.
Kwa maana hiyo, Azam iliyocheza jumla ya mechi 15, ikishinda saba na kutoka sare minane na Yanga iliyokuwa kileleni mwa msimamo na pointi 38, ikishinda 11 na kutoa sare mitano, ndio timu pekee kwa msimu huu ambazo hazijakumbana na kichapo.
MECHI ZA AZAM FC NYUMBANI
(1)-Azam FC 3-0 Mtibwa Sugar
(2)-Azam FC 2-0 TRA
(3)-Azam FC 0-0 Fountain
(4)-Azam FC 3-0 Coastal
(5)-Azam FC 0-0 Singida
(6)-Azam FC 2-0 Mbeya City
(7)-Azam FC 0-0 Yanga
JUMLA YA MECHI-7
USHINDI-4
SARE-3
MABAO YA KUFUNGA-10
MABAO YA KUFUNGWA-0
POINTI-15
MECHI ZA AZAM FC UGENINI
(1)-JKT TZ 1-1 Azam FC
(2)-KMC FC 0-2 Azam FC
(3)-Simba 0-2 Azam FC
(4)-Namungo FC 1-1 Azam
(5)-Pamba Jiji 2-2 Azam FC
(6)-TZ Prisons 0-0 Azam
(7)-Dodoma Jiji 0-3 Azam
(8)-Mashujaa FC 0-0 Azam FC
JUMLA YA MECHI-8
USHINDI-3
SARE-5
MABAO YA KUFUNGA-11
MABAO YA KUFUNGWA-4
POINTI-14