Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sven awatema kikosini Morrison, Bwalya, Ajib

Kocha wa Simba, Sven Vandenbroeck amewaacha nyota wake saba katika safari ya kwenda Mbeya kucheza mchezo wao wa Ligi Kuu dhidi ya Mbeya City.

Simba itashuka dimbani kesho kucheza mechi dhidi ya Mbeya City, mchezo utakaofanyika saa 10 jioni kwenye Uwanja wa Sokoine, huku winga Benard Morrison na Ibrahim Ajib wakiachwa Dar es Salaam.

Katika msafara wa wachezaji uliowasili jana saa saba mchana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Terminal 2, Ajibu, Charles Ilanfya, Kennedy Juma, Morrison, Larry Bwalya na David Kameta hawakuwepo katika msafara huo.

Pia, nyota mpya wa kiganda, Thadeo Lwanga naye hakuwepo katika msafara huo kwani anasubiri ifike Desemba 15 dirisha dogo litakapofunguliwa ndipo aanze kuitumikia timu hiyo.

Alipoulizwa kuhusu wachezaji hao kukosekana, Sven alisema hawana tatizo lolote, lakini amesafiri na wachezaji wanakwenda kucheza mchezo husika.

“Nimeondoka na wachezaji ambao watacheza mechi hii, hao mbona walikuwepo katika mechi zilizopita! Kwahiyo hakuna sababu yoyote nyingine ya kuwaacha zaidi ya hiyo,” alisema kocha huyo raia wa Ubelgiji.

Akizungumzia wapinzani wake, Sven alisema anawahofia kwani licha ya nafasi waliyonayo katika msimamo wa Ligi Kuu, Mbeya City wamekuwa bora katika michezo yao ya mwisho.

“Ni kweli hawapo sehemu nzuri katika msimamo wa Ligi lakini ukiangalia katika mechi zao tano za mwisho hawajafanya vibaya kama walivyoanza, kwahiyo tunajua mchezo utakuwa mgumu,” aliongeza.

Imeandikwa na Thomas Ng'itu na Thobias Sebastian