Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bangala atua usiku Morocco kumalizana na Yanga

YANGA leo inafunga usajili wake baada ya staa wao wa mwisho mpya kutua usiku kuungana na timu hiyo, Mwanaspoti linafahamu.

Akizungumza na Mwanaspoti, beki Yannick Bangala ameliambia kwamba atawasili nchini Morocco leo usiku saa tatu tayari kwa kumalizana kila kitu na timu hiyo iliyopiga kambi jijini Marrakech.

Bangala alisema hiyo ni baada ya kuomba ruhusa ya siku chache kurudi kwao mara moja.

“Nitafika huko Morocco leo usiku (jana), nilikuwa huko ila niliomba muda niende nyumbani mara moja na viongozi wakanikubalia, sasa niko tayari kuanza maisha mapya na Yanga, nakuja.

“Kulikuwa na shida kidogo katika ndege yangu ilikuwa nifike huko tangu juzi, lakini ikashindikana ila sasa mambo yako sawa nakuja haraka hakuna wasiwasi kabisa,” alisisitiza staa huyo ambaye ni mbadala wa Lamine Moro.

Wakati Bangala akisema hayo Mkurugenzi wa Uwekezaji wa GSM ambao ndio wanamwaga fedha kuisajili Yanga, Hersi Said ameliambia Mwanaspoti kwamba: “Tumebakiza mchezaji mmoja tu ambaye bado hajafika na tutamtambulisha tukiwa huku, lakini pia mchezaji wa mwisho kufika atakuwa Khalid Aucho ambaye naye atafika haraka hapa kabla ya wiki hii haijamalizika,”