Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Banka aukubali mziki wa Kagoma

BANKA Pict

Muktasari:

  • Banka alikuwa anacheza kiungo namba sita kama Kagoma jambo linalomshawishi kumfuatilia zaidi aina ya ukabaji wake na kutuliza presha eneo la kati.

KIUNGO wa zamani wa Simba na Yanga, Mohammed Banka amesema anakoshwa na uchezaji wa kiungo mkabaji wa Simba, Yusuf Kagoma anayekaba mtu na mtu jambo ambalo ni gumu kwa wapinzani kupenya eneo analolicheza.

Banka alikuwa anacheza kiungo namba sita kama Kagoma jambo linalomshawishi kumfuatilia zaidi aina ya ukabaji wake na kutuliza presha eneo la kati.

“Aina ya wachezaji kama Kagoma ni wachache kwa nyakati za sasa, ila  kitu ninachoweza kumshauri afanye sana mazoezi yake binafsi yatakayomfanya awe bora na fiti muda wote,” alisema.

“Simaanishi Kagoma asinyumbulike maana hata mimi nilikuwa nafunga kwa kupiga mashuti ya mbali. Kinachonifurahisha zaidi haumpiti kirahisi eneo analokuwepo.”

Huu ni msimu wa kwanza Kagoma kuitumikia Simba aliyosaini miaka mitatu akitokea Singida Fountain Gate  akicheza mechi 12 sawa na dakika 806 ambapo anashindania namba na Fabrice Ngoma, Mzamiru Yassin na Debora Mavambo. “Wakati anasajiliwa Simba hakuwa anatajwa kwa umuhimu mkubwa ila anachofanya kinampa heshima na kutegemewa,” alisema