Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bao la Bwenzi kwa Diarra lilivyofunika mabao ya mastaa hawa

Muktasari:

  • Bwenzi alifunga bao hilo dakika ya 86 ikiwa ni sekunde chache tangu Yanga kufunga bao la sita kupitia kwa Duke Abuya ambapo wakati mashabiki wa Yanga wakiendelea kushangilia bao hilo, ghafla kiungo huyo alianzisha mpira kwa kupiga mpira mrefu ulimshinda nguvu kipa Diarra aliyeusindikiza wavuni.

BAO la kufutia machozi la KenGold lililowekwa kimiani na kiungo, Seleman Rashid ‘Bwenzi’ limekuwa gumzo kwa mashabiki, lakini likiingia kwenye orodha ya mabao makali na bora ya Mwanaspoti yaliyofungwa hadi sasa katika Ligi Kuu Bara msimu huu.

Bwenzi alifunga bao hilo dakika ya 86 ikiwa ni sekunde chache tangu Yanga kufunga bao la sita kupitia kwa Duke Abuya ambapo wakati mashabiki wa Yanga wakiendelea kushangilia bao hilo, ghafla kiungo huyo alianzisha mpira kwa kupiga mpira mrefu ulimshinda nguvu kipa Diarra aliyeusindikiza wavuni.

Katika mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa KMC Complex, Mwenge Dar es Salaam, KenGold ililala kwa mabao 6-1, lakini gumzo ni bao hilo alilotunguliwa Diarra.

Bao hilo lilikuwa ni la tano kwa Diarra kufungwa msimu huu katika Ligi Kuu, lakini likiwa la kwanza kwa Bwenzi aliyetua KenGold katika dirisha dogo lililofungwa hivi karibuni,.

Hilo limekuwa ni bao la kwanza lililofungwa kwa umbali wa mita 50 kwa maana katikati ya uwanja na kulifanya liingine kwenye orodha ya mabao makali kwa mujibu wa Mwanaspoti kwa msimu huu hadi sasa orodha kamili ikiwa hapo chini.


MOHAMED DAMARO (SINGIDA BS)

Kiungo huyu raia wa Guinea anayeichezea Ligi Kuu Bara kwa mara ya kwanza msimu huu, aliifungia Singida Black Stars moja ya bao kali la katikati ya uwanja wakati timu hiyo ilipoibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya KenGold Agosti 18, 2024.

Nyota huyo amejiunga na Singida msimu huu akitokea Hafia FC ya kwao Guinea ambapo bao hilo alilifunga dakika ya 81, ya mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya na kuteka mashabiki baada ya kupiga shuti kali nje ya eneo la 18.


JEAN AHOUA (SIMBA)

Jean Charles Ahoua ni kiungo mpya aliyejiunga na Simba msimu huu akitokea Stella Club Adjame ya  Ivory Coast ambapo alifunga moja ya bao bora nje ya eneo la 18, katika mchezo dhidi ya Fountain Gate, Agosti 25, 2024.

Nyota huyo aliyehusika na jumla ya mabao 12 ya Simba katika Ligi Kuu Bara baada ya kuifungia saba na kuasisti matano, alifunga bao hilo dakika ya 58 katika ushindi wa 4-0, mechi iliyopigwa Uwanja wa KMC Complex Mwenge.

Bao lingine kali la Ahoua alilifunga kwa njia ya ‘Frii-Kii’, katika mchezo uliopigwa Desemba 21, 2024, ambapo timu hiyo ya Simba ilipata ushindi mnono wa mabao 5-2, dhidi ya Kagera Sugar, mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Kaitaba Bukoba.

Ahoua alifunga bao hilo ambalo lilikuwa la pili kwa Simba katika mchezo huo dakika ya 44, baada ya kufanyiwa madhambi na Abdallah Mfuko aliyemuangusha nje kidogo ya eneo la 18 na nyota huyo kupiga mpira uliomshinda kipa, Ramadhan Chalamanda.

Mabao mengine ya Simba katika mchezo huo ulioteka hisia kubwa za mashabiki yalifungwa na beki wa kulia, Shomari Kapombe dakika ya 13 na kiungo, Fabrice Ngoma dakika ya 54, huku Mganda, Steven Mukwala akitupia mawili dakika ya 67 na 85. 


VALENTINO MASHAKA (SIMBA)

Mshambuliaji huyu ni ingizo jipya pia ndani ya Simba aliyojiunga nayo msimu huu akitokea Geita Gold iliyoshuka daraja, ambapo alifunga bao hilo nzuri nje ya eneo la 18, wakati timu hiyo ilipoifunga Fountain Gate mabao 4-0, Agosti 25, 2024.


DICKSON AMBUNDO (FOUNTAIN GATE)

Ambundo alifunga moja ya bao bora msimu huu alipopiga faulu nje ya eneo la 18 na kuzama moja kwa moja wakati Fountain Gate ilipotoka sare ya mabao 2-2, dhidi ya Dodoma Jiji, mchezo uliopigwa Uwanja wa Kwaraa Manyara Septemba 15, 2024.

Nyota huyo alifunga bao hilo dakika ya 86 ya mchezo likiwa ni la kuchomoa baada ya kutanguliwa na Dodoma Jiji kwa mabao 2-1.


NASSOR SAADUN (AZAM FC)

Saadun aliyejiunga na Azam FC msimu huu akitokea Geita Gold amefunga mabao mawili makali ya Ligi Kuu Bara ambapo alianza katika mchezo na KMC uliopigwa Septemba 19, 2024, alipowapiga chenga mabeki sita na kipa kisha kuuzamisha mpira nyavuni.

Nyota huyo alifunga bao hilo dakika ya 60, wakati kikosi hicho cha Azam FC kiliposhinda kwa mabao 4-0, mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa KMC Complex Mwenge jijini Dar es Salaam na kutabiriwa huenda likawa ni moja ya bao bora kwa msimu huu.

Bao lingine la aina hiyo ambalo nyota huyo alilifunga msimu huu, ni lile la ushindi wa timu hiyo wa bao 1-0, dhidi ya Coastal Union Septemba 22, 2024, alipowapiga pia chenga za maudhi mabeki wa ‘Wagosi wa Kaya’ na kuuzamisha mpira wavuni.


YACOUBA SONGNE (TABORA UNITED)

Mshambuliaji huyu aliyewahi kutamba na klabu mbalimbali nchini zikiwemo Yanga na Ihefu ambayo kwa sasa ni Singida Black Stars, amerejea tena na kujiunga na ‘Nyuki wa Tabora’ Tabora United akitokea AS Arta/Solar7 ya Djibouti na kufunga bao bora.

Yacouba alifunga bao kwa shuti kali nje ya eneo la 18 dakika ya 77, wakati kikosi hicho cha Tabora United kilipochapwa mabao 3-1, dhidi ya Fountain Gate, katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi Tabora Septemba 20, 2024.


BEN NAKIBINGE (PAMBA JIJI FC)

Raia huyu wa Uganda alifunga moja ya bao bora msimu huu dakika ya 40, pindi alipopokea pasi safi na kuupiga mpira nje ya eneo la 18, wakati Pamba ikitoka sare ya mabao 2-2 na Mashujaa, mechi iliyopigwa CCM Kirumba Mwanza Septemba 21, 2024.


DAVID ULOMI   (MASHUJAA)

Ulomi ni miongoni mwa nyota waliofunga mabao bora msimu huu ambapo alifanya hivyo alipoifungia timu hiyo dhidi ya Pamba Jiji Septemba 21, 2024, alipoingia akitokea benchi na kuisawazishia Mashujaa na kuufanya mchezo huo kuisha sare ya 2-2.

Mshambuliaji huyo aliyefunga mabao yote mawili ya kusawazisha baada ya Mashujaa kutanguliwa, bao la pili la dakika ya 83 ndilo lililoonekana bora zaidi, baada ya kupiga shuti la mbali lililomshinda kipa wa Pamba, Yona Amos na kuzama wavuni.


EZEKIEL MWASHILINDI (TZ PRISONS)

Mwashilindi aliyerejea tena ndani ya timu hiyo ya Maafande wa Tanzania Prisons msimu huu, baada ya kuachana na Singida Black Stars, alifunga bao nzuri kwa frii-kiki nje ya eneo la 18, wakati kikosi hicho kiliposhinda 3-2, dhidi ya Fountain Gate. 

Nyota huyo alifunga bao hilo likiwa ni la pili kwa Prisons kwenye mchezo huo dakika ya 48, mechi iliyopigwa Uwanja wa Sokoine Mbeya Oktoba 1, 2024, ukiwa ni ushindi wa kwanza kwa kikosi hicho katika Ligi Kuu Bara tangu msimu huu umeanza.


ABDALLAH HASSAN (COASTAL UNION)

Unapotaja mabao bora yaliyofungwa hadi sasa, hutoacha kulitaja la Abdallah Hassan Abdallah wa Coastal Union alilolifunga wakati kikosi hicho cha ‘Wagosi wa Kaya’, kilipoilazimisha Simba sare ya 2-2, mechi iliyopigwa Uwanja wa KMC Oktoba 4, 2024.

Nyota huyo aliyejiunga na Coastal msimu huu akitokea Bandari FC ya Kenya, alifunga bao kali katikati ya uwanja dakika ya 47, baada ya kupiga shuti kali lililomfanya kipa wa Simba Mguinea, Moussa Camara kuuangalia mpira ukizama wavuni mwake.


HERNEST MALONGA (COASTAL UNION)

Bao la nyota huyu raia wa DR Congo alilolifunga dakika ya 71 ya mchezo, lilikatisha kabisa matumaini ya kikosi cha Simba kuondoka na ushindi katika mechi baina yao na Coastal Union na kuifanya kuisha kwa sare ya mabao 2-2, Oktoba 4, 2024.  Malonga aliyejiunga na Coastal Union msimu huu kwa mkopo akitokea Singida Black Stars, alifunga bao hilo nje ya eneo la 18, baada ya kumchungulia kipa wa Simba, Moussa Camara aliyesogea mbele kidogo ya lango lake na kuuzamisha mpira wavuni.


SELEMANI BWENZI (KENGOLD)

Bwenzi aliyetokea benchi alifunga bao katikati ya uwanja baada ya kupiga shuti kali lililozama wavuni kufuatia kushindwa kudakwa na kipa Diarra.

Kiungo huyo alifanya maajabu baada ya kufunga bao la kuvutia kwa shuti kali kutoka katikati ya uwanja wakati wachezaji wa timu zote mbili wakiwa wamezubaa wakijiandaa Kengold ianzishe mchezo baada ya Yanga kufunga bao la sita katika mechi hiyo ya Ligi Kuu Bara.

Badala ya Bwenzi kuanzisha mpira kwa kumpasia mchezaji mwenzake, yeye aliamua kuupiga moja kwa moja langoni kwa Yanga baada ya kumuona kipa Diarra hayupo katika eneo lake na mpira huo kwenda wavuni.

Hili ndio bao ambalo hadi sasa limefungwa kutoka umbali mrefu zaidi, huku pia likiwa bao la tano anafungwa kipa Diarra katika Ligi Kuu Bara msimu huu.

Baada ya bao hilo, Bwenzi amesema aliyatumia vyema makosa aliyokuwa anayafanya kipa huyo wa Yanga na yeye kila siku amekuwa ni mtu wa kujaribu.

“Hii ni moja ya mambo ambayo nimekuwa nikijifunza mazoezini. Diarra ni kipa mzuri lakini kama walivyo wazuri wengine wana changamoto zao, ndiyo nilichokifanya niliangalia udhaifu wake nikautumia, unajua pale alikuwa mbele sana, ni goli zuri lakini makosa yake ndiyo yamechangia.

“Mimi kama mchezaji nilipokuwa naagalia niliona kama vile alikuwa anaomba maji (kwa wasaidizi wa timu waliokuwa pembeni ya uwanja), hivyo alishaondoka langoni kwake ndiyo maana nikaamua kujaribu na kweli nimefanikiwa kufunga,” anasema Bwenzi ambaye baada ya mechi baadhi ya mashabiki walionekana kumpongeza na kumpa pesa wakiwamo waliovaa jezi za Yanga.