Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Beimbaya: Malengo ni kuiweka B19 mbali na Play-Off

BEI MBAYA Pict

Muktasari:

  • Beimbaya aliyewahi kuifundisha pia Pan Africans, kwa sasa ameiongoza B19 FC ikishika nafasi ya 12 na pointi 21, baada ya timu hiyo kushinda mechi tano, sare sita na kupoteza 12na safu ya ushambuliaji imefunga mabao 20 na kuruhusu 37.

KOCHA Mkuu wa B19 FC, Twaha Beimbaya amesema mwenendo wa timu hiyo kwa sasa unaridhisha na unawaweka katika malengo ya kukipigania kikosi hicho kutoka nafasi za kucheza mechi ya mtoano (Play-Off), ili kujiweka katika mazingira bora zaidi.

Akizungumza na Mwanaspoti, Beimbaya amesema malengo ya timu hiyo kwa sasa ni kupambana kubakia Ligi ya Championship kwa msimu ujao, licha ya ushindani mkubwa uliopo kutoka kwa wapinzani wao, hususani kwa mechi hizi za kumalizia msimu huu.

"Lengo letu ni kutoka kabisa nafasi za kucheza mchujo (Play-Off), ndio maana tunataka kupambana katika mechi zetu saba zilizobakia, tunatambua ushindani ni mkubwa sana kutokana na malengo na mahitaji ya kila mmoja wetu," amesema Beimbaya.

Kocha huyo aliyewahi kuifundisha Kiluvya United kwa sasa Barberian, amepewa jukumu la kukiongoza kikosi cha B19 zamani Tanesco kwa mkataba wa miezi sita, baada ya uongozi wa timu hiyo kuachana na Babou Salim kwa makubaliano ya pande mbili.

Beimbaya aliyewahi kuifundisha pia Pan Africans, kwa sasa ameiongoza B19 FC ikishika nafasi ya 12 na pointi 21, baada ya timu hiyo kushinda mechi tano, sare sita na kupoteza 12na safu ya ushambuliaji imefunga mabao 20 na kuruhusu 37.