Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bondia Mnemwa aomba msaada wa matibabu ili arudi ulingoni

Muktasari:

  • Mnemwa alipatwa na tatizo la damu kuvilia kwenye ubongo baada ya kupigwa KO katika raundi ya tatu ya pambano alilocheza na Ally Sewe kwenye pambano lililofanyika Januari 24, 2025 katika ukumbi wa Mrina uliopo Manzese Tiptop jijini Dar es salaam.

Bondia Mohammed Mnemwa ameomba msaada kwa Serikali, vyama vya mchezo wa ngumi pamoja na wadau kumsaidia kulipa gharama za matibabu anayopatiwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili.

Mnemwa alipatwa na tatizo la damu kuvilia kwenye ubongo baada ya kupigwa KO katika raundi ya tatu ya pambano alilocheza na Ally Sewe kwenye pambano lililofanyika Januari 24, 2025 katika ukumbi wa Mrina uliopo Manzese Tiptop jijini Dar es salaam.

Katika mahojiano aliyofanyiwa na TBC bondia Mnemwa amepeleka kilio chake kwa wadau ili apate msaada aweze kupona na kurudi tena ulingoni.

"Mimi kwa hali yangu nilikua naomba watu wajitokeze serikali kama hivyo vyama vya ngumi wanisaidie kwa gharama zitakazotajwa hapa ili niendelee kurudi kwenye michezo yangu kwasababu ngumi ndio maisha yangu ambayo nimejichagulia.

"Kama misaada kama mtu yeyote mwenye uwezo watu wanaonijua waandaaji wa mapambano wasimamizi lazima wasogee kama kuja kuniona na watahusika na chochote kitu ili mwenyewe niweze kuinuka tena niendelee na shughuli zangu sasa hivi nasikia maumivu kwenye kichwa," amesema Mnemwa.

Bondia huyo kwasasa anapatiwa matibabu kwenye taasisi ya mifupa MOI iliyopo chini ya hospital ya Taifa ya Muhimbili ambapo baada ya vipimo alivyofanyiwa awali aligundulika na tatizo la damu imevilia kwenye ubongo.