Bondia Swanga apoteza Madola

Dar es Salaam. Bondia Haruna Swanga ameaga mashindnao ya Jumuiya ya Madola baada ya kupigwa kwa pointi za majaji 5-0 kwenye uzani wa juu.
Swanga alipoteza pambano hilo leo asubuhi dhidi ya Naman Tanwar wa India baada ya kumaliza raundi zote tatu na majaji kutoa ushindi kwa Tanwar wa pointi 30-29, 30-25, 30-26, 30-24, 30-25 na 30-24.
Bondia huyo anakuwa Mtanzania wa pili kufanya vibaya baada ya jana muogeleaji Hilal Hilal kushindwa kuingia fainali ya mita 50 freestyle.
Baadaye mchana leo, Bondia Suleiman Kidunda atapanda ulingoni kuzichapa na Mkenya, Edwin Owuor.
Wakati kesho, Jumamosi mabondia Kassim Mbutike na Ezra Paul watapanda ulingoni kuzichapa kwenye hatua ya 16 bora.
Riadha wenyewe wataanza kutupa kete ya kwanza kwenye mbio fupi Jumapili ambapo Ali Gulam atachuana kwenye mbio za mita 100 na 200.