Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Camara wa Simba amuibua Idd Pazi

Camara Pict
Camara Pict

Muktasari:

  • Camara aliyesajiliwa na Simba msimu huu akitokea AC Horoya ya Guinea, amekuwa mhimili wa ukuta wa timu hiyo kwa msimu huu akiwafunika makipa wengine wazawa akiwamo, Aishi Manula, Hussein Abel na Ally Salim. Katika mechi 18 ilizocheza Simba amedaka zote na kuvuna clean sheet 14.

UMAHIRI wa Moussa Camara 'Spider' katika milingoti mitatu ya Simba, akiwa amebakisha clean sheet moja tu kwa sasa kuifikia rekodi iliyowekwa Ligi Kuu Bara msimu uliopita kiasi cha kumpa tuzo aliyekuwa kipa wa Coastal Union, Ley Matampi, umemuibua nyota wa zamani nchini, Idd Pazi 'Father'.

Camara aliyesajiliwa na Simba msimu huu akitokea AC Horoya ya Guinea, amekuwa mhimili wa ukuta wa timu hiyo kwa msimu huu akiwafunika makipa wengine wazawa akiwamo, Aishi Manula, Hussein Abel na Ally Salim. Katika mechi 18 ilizocheza Simba amedaka zote na kuvuna clean sheet 14.

Idadi hiyo imemfanya Camara maarufu kama Spider au Pip Pin, kulingana na zile alizovuna kipa namba moja wa Yanga, Djigui Diarra msimu uliopita alipocheza mechi 21 wakati Camara akicheza 18 pekee.

CAM 01

Pia Camara amebakisha cleansheet moja kuifikia rekodi ya Matampi aliyetwaa tuzo ya Kipa Bora wa msimu uliopita alipomaliza na cleansheet 15 kwenye mechi 25 alizocheza, huku uhodari wake ukimtoa Father mafichoni na kumsifia.

Mbali na kumsifia, kipa huyo wa zamani wa kimataifa aliyewahi kutamba na Simba, Majimaji Songea, Pilsner na Al Hilal ya Sudan na timu ya taifa, Taifa Stars, alisema anachokifanya Camara ni muendelezo ya rekodi ya makipa bora kuwepo Simba, akikumbushia jina la Tanzania One.

Father alisema jina la Tanzania One litaendelea kuibeba Simba, kwani kwa miaka mingi imekuwa na jicho la kuona makipa bora akikumbushia enzi zake na wengine waliopita Msimbazi wengi wakiwa wazawa na kulivaa jina hilo la Tanzania One ambalo liliasisiwa miaka ya 1980 enzi aking'ara.

CAM 02

Ikumbukwe kipa wa kwanza kuitwa Tanzania One, alikuwa ni yeye Father baada ya kuanza kuichezea Stars akiwa panga pangua kuanzia 1982 hadi 1992 kutokana na umahiri aliokuwa nao hadi katika majukumu ya klabu ya Simba wakampachika jina hilo.

"Makipa Tanzania One wote walitokea katika klabu ya Simba ambao eneo hilo waliwapa nafasi wazawa kuliko wageni na ili uwe na sifa ya Tanzania One lazima uwe panga pangua katika klabu yako na timu ya taifa," alisema Father na kuongeza.

"Nakumbuka ilipofika mwaka 1992 nilimchukua Mohammed Mwameja kutoka Coastal Union na kumpeleka Simba, alikuwa na hofu  kama anaweza akadaka mbele yangu, nilimwambia nazeeka anapaswa abadili yeye Tanzania One na ikawa hivyo.

CAM 02 (1)

"Baadaye akaja Juma Kaseja, Aishi Manula ambaye jina linafia mikononi mwake lakini kwa umri wake bora atafute timu nyingine bado kwani ana uwezo wa kurejesha heshima ya Tanzania One na akaliacha kwa mtu mwingine, binafsi Abuutwalib Mshery akipata nafasi anastahili, ingawa sijui waliomzunguka na yeye mwenye anakionaje kipaji chake," alisema Father aliyewahi kucheza soka la kulipwa Indonesia katika klabu ya Persiraja Banda Aceh, huku rekodi yake ya kufunga katika Dabi ya Kariakoo aliyoiweka mwaka 1984 ilikuja kufikiwa na Kaseja katika ushindi wa mabao 5-0 iliyopata Simba, Mei 6, 2012 alipofunga penalti.