Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Daraja la kwanza Dar ubora, vipaji vyafunika

Daraja Pict

Muktasari:

  • Zikiwa tayari zimeshapanda daraja na msimu ujao zitacheza michuano ya Ligi ya Kikapu Dar es Salaam (DBL) miamba hiyo ilionyeshana kazi na mshindi kupatikana kwa mbinde mwisho Polisi ikiibuka na pointi 64-60.

USHINDANI na viwango bora kutoka kwa nyota wa Polisi na Stein Warriors katika robo zote nne, vimeifanya fainali ya kikapu, Ligi Daraja la Kwanza Dar es Salaam kuwa moja ya michezo iliyovutia zaidi katika michuano hiyo msimu huu.

Zikiwa tayari zimeshapanda daraja na msimu ujao zitacheza michuano ya Ligi ya Kikapu Dar es Salaam (DBL) miamba hiyo ilionyeshana kazi na mshindi kupatikana kwa mbinde mwisho Polisi ikiibuka na pointi 64-60.

Ushindani huo ulisababisha majeruhi, baada ya wachezaji wawili Lawi Mwambasi wa Polisi na Mwinyipembe Jumbe wa Stein wachanike  katika paji la uso baada ya kugongana.

Stein iliingia uwanjani na kumbukumbu ya kufungwa pointi 71-58 na kutaka kulipa kisasi, lakini ilizidiwa ujanja na Polisi huku nyota na mchezaji bora wa mashindano hayo Mwambasi akisema kilichowabeba ni nidhamu ya wachezaji ndani na nje ya uwanja.

Pia alisema hawakuwa wakionywa sana na waamuzi kama timu nyingine kutokana na kukiuka taratibu na kanuni za mchezo na waliwaheshimu wapinzani wao na walijitoa kuipambania timu yao na mazoezi na kukaa pamoja muda mrefu vilichangia.


DA 01

GODFREY AZUA GUMZO

Katika michuano hiyo, mmoja wa watu waliovutia ni kocha wa Kurasini Heat, Brian Godfrey kutokana na umri wake mdogo (miaka 12) akiwaongoza wachezaji waliomzidi umri, huku akiiwezesha kumaliza nafasi ya tatu.

Kocha huyo aliyekuwa akitekeleza vyema majukumu yake ikiwamo kuhakikisha wanatendewa haki na waamuzi, alisema katika ligi hiyo amejifunza mengi ikiwamo kuwa mvumilivu.

“Uvumilivu pamoja na kwa wachezaji, mimi ni binadamu naweza nikakosea kutoa maelekezo kwao,” alisema Godfrey na kuongeza licha ya umri wake mdogo, lakini wachezaji wanamheshimu na kufuata maelekezo yake.


DA 03

MKOSA MSIFIA

Kocha mkuu wa timu hiyo na Mchenga Star, Amin Mkosa alisema alimwona Godfrey akihudhuria mazoezi ya Kurasini Heat wakati akiifundisha kwenye Uwanja wa Bandari, Kurasini na kugundua ana kipaji na kumfanya awe kocha.

Pia anasema alikuwa akiwafundisha watoto wenzake kwa lengo la kuwafanya waupende mchezo huo na kutokana na kuvutiwa naye aliamua amtambulishe kwa wachezaji na viongozi wa timu hiyo.

“Nilipomwona niligundua ana uwezo wa pekee, tofauti na watoto wengine katika kuelewa mchezo wa kikapu na viongozi walimtaka azingatie pia masomo na asipofanya hivyo hawatamruhusu kuifundisha timu hiyo," alisema Mkosa.

Kamishna wa ufundi na makocha TBF, Robert Manyerere alisema Godfrey ni kijana mdogo aliyeamua kujikita kwenye ukocha na anafanya vyema chini ya usimamizi wa timu hiyo waliomwamini na kuwa msaidizi.

“Ni wazi ana kipaji cha uongozi ambacho kupitia ukocha huu kitaimarika, ni matarajio yangu kipaji kikisimamiwa vizuri na kuendelea kupata sapoti, atakuwa kocha mwenye ujuzi,” alisema Manyerere.

DA 04

Alisema kitendo cha kuamua kufanya mafunzo ya ukocha na uamuzi katika fani hii ni jambo kubwa sana kwake na kwa tasnia hii na hata makocha alioshiriki naye mafunzo walishangaa kutokana na umri wake.

Alisema alionyesha uwezo mkubwa wakati wa kuwasilisha mada mbalimbali darasani na kujibu maswali na hata katika mafunzo kwa vitendo uwanjani.


DA 02

NGAIZA AKUBALI MZIKI WA KURASINI

Nyota wa timu ya Taifa  na Vijana 'City Bulls', Fotius Ngaiza  alisema amevutiwa na kiwango cha Kurasini Heat baada ya kuiona ikiifunga Mlimani B.C kwa pointi  56-48, katika mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu.

Alisema timu hiyo iliyoundwa na baadhi ya vijana chipukizi, ilicheza kwa ushirikiano mkubwa ingawa ameitaka kufanya marekebisho kidogo ya kusajili kabla ya kuanza Ligi ya Mkoa wa Dar es Salaam (BDL).

“Ligi ya BDL ni ngumu na baadhi ya timu zimekuwa zikisajili  wachezaji wa kigeni wenye uwezo mkubwa na kama utajiandaa utakuwa ukichezea tu vichapo,” alisema Ngaiza.

Kuhusu ligi hiyo, alisema ilikuwa ngumu sana na yenye ushindani mkubwa na ubora ulianza kuonekana zaidi hatua ya robo fainali kutokana na kila timu kucheza kwa lengo la kufuzu nusu fainali.