Fountain Gate Princess shida ni washambuliaji

Muktasari:
- Mashindano hayo yalifanyika Machi 4 hadi 7 yakijumuisha timu nne ambazo ni Yanga Princess iliyochukua ubingwa kwa kuitandika JKT Queens mabao 3-1, Simba Queens iliyomaliza nafasi ya tatu na Fountain.
KOCHA wa Fountain Gate Princess, Camil Mirambo amesema mashindano ya Samia Women Cup yaliyofanyika mkoani Arusha yamemuonyesha mwanga wa eneo lipi anapaswa kulifanyia kazi kwa haraka.
Mashindano hayo yalifanyika Machi 4 hadi 7 yakijumuisha timu nne ambazo ni Yanga Princess iliyochukua ubingwa kwa kuitandika JKT Queens mabao 3-1, Simba Queens iliyomaliza nafasi ya tatu na Fountain.
Akizungumzia hilo, Mirambo alisema kucheza na Yanga na Simba kumempa mwanga wa kufanya ligi itakaporejea kuhakikisha eneo la ushambuliaji na ulinzi linapunguza makosa.
Aliongeza kuwa ukikutana na timu bora kama hizo zinamuonyesha timu hiyo ina udhaifu eneo lipi na fasta kuanza kufanyia kazi.
“Mechi zile mbili zimeonyesha udhaifu wetu kwenye eneo la ushambuliaji ambalo halikuwa na ubora hata ulinzi lilipata tabu kukutana washambuliaji wa Simba na Yanga ambao wana matumizi mazuri ya nguvu na nafasi.
“Baadhi ya wachezaji wetu wako kwenye majukumu ya timu ya taifa ‘ Serengeti Girls’ hivyo kwa kiasi fulani timu ilibadilika kimfumo ingawa sio sababu kubwa lakini tumeyaona makosa na tutayafanyia tazi.”