Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Gamondi atia neno ushindani Muungano Cup

GAMONDI Pict

Muktasari:

  • Timu zingine mbili za pande hizo mbili zilikuwa uwanjani jana na Singida Black Stars ilikuwa ikipambana na Mlandege wakati Simba ikiwa mgeni wa Mafunzo kwenye michezo mingine ya robo fainali.

KOCHA wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Miguel Gamondi, yupo hapa Zanzibar akiwa na ratiba zingine, lakini alipoangalia mechi mbili tu za Kombe la Muungano akatoka na mambo matatu juu ya ushindani wa timu shiriki.

Akizungumza na Mwanaspoti, Gamondi amesema hana shida na mashindano hayo, lakini jambo la kwanza alilogundua ni utofauti wa ubora kwa timu za Zanzibar na zile zinazotoka Ligi Kuu Bara.

Gamondi amesema kuna utofauti mkubwa kwa vikosi vinavyotoka ligi hizo mbili, akisema bado timu za Zanzibar kiwango chake kipo chini hatua ambayo zimejikuta zikipoteza kirahisi.

“Kitu ambacho nimekiona ni utofauti mkubwa wa ushindani, huwezi kukwepa kusema hili, kuna tofauti kubwa sana ukiangalia timu za kutoka hapa Zanzibar zimeonekana kama uwezo wake upo chini kulinganisha na zile zinatoka Bara,” amesema Gamondi.

“Hizi ni timu zinazotoka kucheza ligi mbili tofauti, nadhani kuna haja ya makusudi kupandisha ubora wa ligi ya hapa Zanzibar ili kutoa ushindani mkubwa wakati mwingine.

“Unaweza kuona timu za Bara zimefanya rotesheni kubwa kwenye vikosi vyao, lakini bado zimeweza kushinda vizuri, maana yake wachezaji wake ni bora sana kiushindani kuliko hawa wa hapa.”

Kwenye mechi mbili za kwanza za mashindano haya yanayoendelea kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar, timu mbili za Bara zimetinga nusu fainali kirahisi na Yanga ilitangulia kuichapa Muembe Makumbi 4-0, kisha Azam kuiondosha KVZ kwa mabao 2-0.

Timu zingine mbili za pande hizo mbili zilikuwa uwanjani jana na Singida Black Stars ilikuwa ikipambana na Mlandege wakati Simba ikiwa mgeni wa Mafunzo kwenye michezo mingine ya robo fainali.

Aidha Gamondi aliongeza, amekutana na makocha wa timu za Zanzibar na kuzungumza nao mambo ambayo wanatakiwa kuyafanya katika kuinua vipaji vya wachezaji wa hapa.

“Nilikuja hapa kwa kazi nyingine tofauti ya kukutana na makocha wa Zanzibar, kuna mambo tumepeana ili kuhakikisha wanakwenda kuinua vipaji vya ligi ya hapa,” amesema Gamondi.