Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Gets Program kurudi upya WPL

Gets Pict

Muktasari:

  • Timu hiyo haikuanza vyema ligi ikipitia changamoto ya ukata uliosababisha baadhi ya wachezaji kutimka kambini na kutafuta changamoto sehemu mbalimbali.

KOCHA wa Gets Program iliyopanda daraja msimu huu, Aristides Ngowi licha ya kuwa na wachezaji wengi vijana ambao hawana uzoefu na ligi, lakini wanapambana jambo linalowapa motisha ya kujipanga upya kipindi hiki cha mapumziko.

Timu hiyo haikuanza vyema ligi ikipitia changamoto ya ukata uliosababisha baadhi ya wachezaji kutimka kambini na kutafuta changamoto sehemu mbalimbali.

Wachezaji hao ni pamoja na Zubeda Mgunda, Diana Mnally, Protasia Mbunda waliotimka Yanga Princess na Zainabu Mohamed aliyetimkia Mashujaa Queens.

Ngowi alisema kama kocha anapambana na mabinti wadogo ambao wengi wamesajili kutoka Ligi ya Mkoa ambao bado hawana uzoefu na ligi akiamini wakipata muda kidogo watakuwa bora.

Aliongeza wanapaswa kukaza buti kwenye mechi zilizosalia ili kuhakikisha timu hairudi Ligi Daraja la Kwanza ikiwemo kushinda karibu kila mchezo.

"Vijana bado wadogo, hata hivyo wanajitahidi sana, tumepitia kipindi kigumu hapa kati lakini wanapambana sana, mipango ni kubaki Ligi Kuu na si kingine," alisema Ngowi.