Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hesabu za vidole zaanza Championship

HESABU Pict

Muktasari:

  • Hadi sasa zikiwa zimechezwa raundi 23, zimebaki saba pekee sawa na dakika 630 za kuamua timu mbili za kupanda Ligi Kuu na mbili kushuka moja kwa moja, huku nafasi ya tatu na nne zikicheza play off ya kupanda na za nafasi ya 11 hadi 14 zikipambania kubaki.

WAKATI upepo ukionekana kukata kwa Barberian na Hausung kwenye Ligi ya Championship, hesabu za vidole zimeanza kwa timu za Geita Gold na Kagera Sugar kwenye vita ya kurejea Ligi Kuu Bara, huku mtifuano ukinoga nneo bora.

Hadi sasa zikiwa zimechezwa raundi 23, zimebaki saba pekee sawa na dakika 630 za kuamua timu mbili za kupanda Ligi Kuu na mbili kushuka moja kwa moja, huku nafasi ya tatu na nne zikicheza play off ya kupanda na za nafasi ya 11 hadi 14 zikipambania kubaki.

CHAMP 01

Geita Gold inacheza Ligi ya Championship kwa msimu wa pili mfululizo, huku Kagera Sugar ikiwa ni msimu wa kwanza, ambapo timu hizo zimeonesha ubora, ushindani na nia ya kurudi Ligi Kuu kwa matokeo waliyonayo.

Vinara wa ligi hiyo Geita Gold wenye pointi 58 na Kagera Sugar wenye 55, wameanza hesabu za vidole kwa michezo iliyobaki wakisaka japo ushindi wa michezo mitano tu ili kujihakikishia kurejea Ligi Kuu.

CHAMP 02

Hata hivyo, Mbeya Kwanza waliopo nafasi ya tatu kwa pointi 51, Polisi Tanzania nafasi ya nne kwa pointi 48 na Transit Camp pointi 48 zinakimbiza kimyakimya, zikiwa na matumaini ya kufanya kweli.

Kati ya mechi saba ilizonazo Geita Gold, itacheza nne nyumbani dhidi ya Mbuni, TMA, Songea United na Bigman, huku ugenini ikizifuata Kagera Sugar, KenGold na Stand United.

Kwa upande wa Kagera Sugar, itacheza tano nyumbani dhidi ya Mbuni, Geita Gold, KenGold, Gunners na Mbeya Kwanza na kutoka michezo miwili tu dhidi ya TMA na Songea United.

CHAMP 03

Kocha Mkuu wa Geita Gold, Zuberi Katwila, amesema bado ligi ni ngumu na vita ya kupanda si rahisi japokuwa anashukuru vijana wake wanapambana na uongozi unatoa sapoti hali inayoongeza morali kikosini.

“Kila mchezo una hesabu zake na kubwa zaidi ni kupambania pointi tatu, ushindani ni mkali kwa kila timu tunayokutana na matarajio yetu ni kuona tunarudi Ligi Kuu, tunaheshimu wapinzani kila mechi,” amesema kocha huyo.

CHAMP 04

Naye Kocha Mkuu wa Polisi Tanzania, Mbwana Makata amesema wanaendelea kupambana hadi mwisho wa ligi akikiri upinzani kuwapo kwa timu pinzania akitoa matumaini kuwa wanaitaka Ligi Kuu.

“Dhamira yetu ni kuendelea kupambana kwakuwa mechi bado zipo, kiu yetu ni kuona tunarudi Ligi Kuu, vijana wanapambana na nishukuru sapoti ya menejimenti,”  amesema kocha huyo.