Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Issa Abushehe: Polisi Tanzania sasa ni mwendo wa nne bora

ABUSHEE Pict

Muktasari:

  • Polisi iliyoshuka daraja kutoka Ligi Kuu Bara hadi Ligi ya Championship msimu wa 2022-2023, kwa sasa imecheza mechi 23, ikishinda 14, sare sita na kupoteza tatu tu, ikishika nafasi ya nne na pointi 48, huku ikifunga mabao 38 na kuruhusu 17.

KIUNGO mshambuliaji wa maafande wa Polisi Tanzania, Issa Abushehe 'Messi' amesema kwa sasa timu hiyo ina morali mkubwa kuanzia kwa wachezaji, viongozi na benchi la ufundi, kutokana na mwenendo mzuri katika Ligi ya Championship.

Akizungumza na Mwanaspoti, Abushehe amesema raundi ya kwanza ilikuwa ngumu kwa kikosi hicho kutokana na kuandamwa na matokeo mabaya, ingawa upepo huo mbaya umeshaondoka na sasa wako tayari kwa ajili ya kupigania upya nafasi nne za juu.

"Kilichokuwa kinatuangusha raundi ya kwanza ni safu ya ushambuliaji kukosa umakini wa kumalizia nafasi za kufunga, baada ya hapo tulikaa chini na kujifanyia tathimini wenyewe na kusahihisha makosa tuliyokuwa nayo mwanzoni," amesema Abushehe.

Nyota huyo amejiunga na Polisi baada ya kuachana na Namungo aliyojiunga nayo dirisha dogo la Januari 2025, ikiwa ni muda mfupi tangu avunje mkataba wake wa miezi sita na KVZ, inayoshiriki Ligi Kuu ya Zanzibar kwa makubaliano ya pande mbili.

Kiungo huyo alijiunga na KVZ kwa msimu wa 2024-2025, akitokea Biashara United ya mkoani Mara iliyokuwa inashiriki Ligi ya Championship, huku akiwahi pia kuzichezea timu mbalimbali zikiwemo za Coastal Union na Al Mokawloon Al Arab ya Misri.

Polisi iliyoshuka daraja kutoka Ligi Kuu Bara hadi Ligi ya Championship msimu wa 2022-2023, kwa sasa imecheza mechi 23, ikishinda 14, sare sita na kupoteza tatu tu, ikishika nafasi ya nne na pointi 48, huku ikifunga mabao 38 na kuruhusu 17.