Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kaizer ya ng’ang’ana na Fei Toto, yafikia hapa!

Muktasari:

  • Kaizer inayonolewa na kocha wa zamani wa Yanga, Nasreddine Nabi aliyewahi kumnoa nyota huyo, imewasilisha ofa mpya kwa Azam FC

KAMA unadhani klabu ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini imeamua kumpotezea kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Feisal Salum ‘Fei Toto’, baada ya ofa yao waliyoiwasilisha Azam FC, pole yako, kwani mabosi wa klabu hiyo wameamua kurudi kivingine Chamazi wa kudaiwa kuongeza mzigo.

Kaizer inayonolewa na kocha wa zamani wa Yanga, Nasreddine Nabi aliyewahi kumnoa nyota huyo, imewasilisha ofa mpya kwa kuongeza Dola 15,000 katika ofa ya awali ili kuinasa saini ya Fei Toto ili kwenda kuiongezea ufanisi zaidi safu ya ushambuliaji ya timu hiyo.

Taarifa kutoka Kaizer Chiefs ni kwamba uongozi wa klabu hiyo umetuma ofa ya pili ya Dola 350,000 (Sh 884 milioni) ambayo bado Azam imeweka ngumu kuikubali ndipo Wasauzi hao wakajiongeza kidogo.

Kaizer sasa imewasilisha ofa mpya ya tatu ya Dola 365,000 (Sh 922 milioni) ikiwa katika siku za mwisho kabla ya kufungwa kwa usajili wa dirisha dogo nchini humo.

Azam inataka Kaizer Chiefs itoe kiasi kisichopungua dola 500,000 (Sh 1.2 Bilioni) kumuachia kiungo huyo wa zamani wa Yanga.

Taarifa zaidi zinasema hata Fei Toto akitaka kuachana na Azam kwa kuununua mkataba alionao na matajiri hao wa Chamazi atatakiwa kutoa kiasi hicho cha Dola 500,000 kisha atakuwa huru kwenda klabu aitakayo.

Bado Azam haijawajibu Kaizer Chiefs ambapo Wasauzi hao wanataka kufunga dirisha dogo la usajili kwa kumshusha kiungo huyo ambaye ameshawaambia mabosi wake kwamba anataka kuondoka nchini.

“Fei amesha-mwambia (CEO) Ofisa Mtendaji Mkuu, Abdukarim Amin ‘Popat’ kwamba anataka kuondoka kwenda kujaribu maisha nje ya nchi na wala hataki kuondoka vibaya ndani ya Azam unajua walikubaliana wakati anakuja hapa kwamba kama ikitokea timu nzuri ambayo itamvutia na kufikia maslahi ya klabu wamuache akajaribu kucheza nje,” alisema bosi mmoja ndani ya Azam.

Aliyeongeza; “Azam imeshampa mkataba mpya wa kufuru Fei, lakini bado hajakubali kusaini akisema tumpe muda lakini hapa inaonyesha ni wazi kwamba akili yake ipo nje, hata ukimueleza ofa yoyote ya ndani hataki kusikia.”