Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kapombe aitaka ndoo Afrika

Muktasari:

  • Kapombe amecheza mara kadhaa katika hatua za juu za michuano ya kimataifa akifika robo fainali mara tatu kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika (misimu ya 2020–21, 2022–23 na 2023–24), na hii itakuwa mara yake ya pili katika Kombe la Shirikisho huku ile ya kwanza ikiwa msimu wa 2021–22.

BEKI mahiri wa Simba, Shomary Kapombe ameweka wazi kwamba ndoto yake kubwa kwa sasa ni kutwaa ubingwa wa michuano ya kimataifa, iwe Ligi ya Mabingwa Afrika au Kombe la Shirikisho.

Kapombe amecheza mara kadhaa katika hatua za juu za michuano ya kimataifa akifika robo fainali mara tatu kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika (misimu ya 2020–21, 2022–23 na 2023–24), na hii itakuwa mara yake ya pili katika Kombe la Shirikisho huku ile ya kwanza ikiwa msimu wa 2021–22.

Jumla Simba hii ni robo fainali ya sita katika michuano ya CAF kuanzia msimu wa 2018-2019 huku Kapombe akicheza zote.

“Ubingwa wa Afrika ni jambo ambalo limekuwa likinitatiza akili yangu kwa muda mrefu,” alisema Kapombe na kuongeza.

“Kabla sijamaliza safari yangu ya soka, nataka kuandika historia na klabu yangu Simba. Hii ni ndoto yangu, na kila msimu unavyoenda, kiu yangu ya kutwaa ubingwa wa Afrika inazidi kuwa kubwa.

“Kufika robo fainali ni jambo la kujivunia, lakini Simba inahitaji zaidi ya hatua hii. Tunahitaji kuendelea kupambana ili kuandika historia. Yapo mabadiliko kwenye timu yetu, na ndiyo maana nina imani kubwa kuwa tunaweza kufanikisha hili.

“Hii ni nafasi yetu ya kufanya kile ambacho hatujawahi kufanya kutwaa ubingwa wa Afrika.

“Najua kuwa safari ya mafanikio si rahisi, lakini kama tunaendelea na juhudi, hatutashindwa.”

Kapombe amecheza mechi 40 za kimataifa na Simba, akifunga mabao matatu na kutoa asisti tatu, huku mchango wake ukiwa mkubwa hasa katika safu ya ulinzi na kushambulia kwa kupanda mbele mara kwa mara.