Kaze amtega Metacha kisa bao la Dodoma

Muktasari:
KOCHA mkuu wa Yanga, Cedric Kaze amesema hakufurahishwa na bao alilofungwa kipa wake Metacha Mnata katika mchezo wao dhidi ya Dodoma uliomalizika wakishinda 3-1.
KOCHA mkuu wa Yanga, Cedric Kaze amesema hakufurahishwa na bao alilofungwa kipa wake Metacha Mnata katika mchezo wao dhidi ya Dodoma uliomalizika wakishinda 3-1.
Metacha alifungwa bao hilo dakika ya 3 ya mchezo baada ya winga wa Dodoma, Dickson Ambundo kupiga krosi na yeye kuudaka mpira kisha akauachia chini na mshambuliaji Seif Karie aliupiga mpira kwa kichwa na kwenda wavuni huku likionekana ni goli la kizembe ambalo amefungwa.
Baada ya goli hilo mashabiki na benchi la ufundi la Yanga walionekana kupoa lakini wachezaji wa ndani walitumia uzembe wa wachezaji wa Dodoma kujilinda na wao wakasawazisha na baadaye kufunga magoli mawili mengine.
“Makosa ni kawaida lakini kosa ambalo linasababisha goli ni baya, kipa ana uzoefu, nafikiri yeye mwenyewe ameona nini kilichotokea,”
Kaze alisema Metacha anatakiwa asijione amamemaliza bali aendeleze kiwango chake ambacho alikuwa awali katika mechi zilizopita.

“Nadhani anatakiwa aendeleze kiwango chake alichokuwa nacho, hapaswi kuridhika kabisa bali anatakiwa kubakia katika levo yake kubwa zaidi.”
Kaze aliongeza kwa kusema “Uzuri ni kwamba katika mchezo hu wachezaji wenzake walipambana na kurejesha magoli.”