Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

KenGold yamliza Cabaye Bara

CABAYE Pict

Muktasari:

  • Kengold iliyopanda daraja msimu huu na kushuka kwa kuvuna pointi 16 tu katika mechi 27, baada ya kupoteza mechi nne mfululizo zilizopita mbele ya Azam (2-0), Dodoma Jiji (3-0), Tanzania Prisons (3-1), na Coastal Union (2-1).

KIUNGO wa KenGold, Abdallah Masoud 'Cabaye' amefunguka kuhusu kuumizwa kwa kitendo cha timu hiyo kushuka daraja, licha ya kubakiwa na michezo mitatu kabla ya kumalizika kwa msimu huu wa 2024/25.

Kengold iliyopanda daraja msimu huu na kushuka kwa kuvuna pointi 16 tu katika mechi 27, baada ya kupoteza mechi nne mfululizo zilizopita mbele ya Azam (2-0), Dodoma Jiji (3-0), Tanzania Prisons (3-1), na Coastal Union (2-1).

Hii ni mara ya kwanza kwa timu anayoichezea Cabaye kushuka daraja, jambo linaloonekana kumgusa kiungo huyo mkabaji na kabla ya kujiunga nayo alitokea Azam na KMC, lakini sasa anashuhudia kipindi kigumu zaidi cha maisha yake ya soka.

"Licha ya kwamba tumekutana na changamoto nyingi msimu huu, kuwa sehemu ya timu inayoshuka daraja ni jambo la maumivu makubwa kwangu na kwa wachezaji wenzangu. Tumepambana, lakini hatujafanikiwa," alisema Cabaye.

"Hii ni mara yangu ya kwanza kushuhudia kushuka daraja kwa timu ninayoichezea na ni jambo linalonifanya nijiulize maswali mengi."

Hata hivyo, licha ya kukabiliwa na adhabu ya kusimamishwa kwa kosa la utovu wa nidhamu pamoja na wachezaji wenzake kama Seleman Bwenzi, Steven Duah, James Msuva na Uhuru Seleman, ambaye ni kocha wa viungo, Cabaye ameapa kubaki mstari wa mbele kwa ajili ya kuwasapoti wachezaji wenzake katika michezo iliyosalia.

"Haijalishi hali ilivyo, mimi ni mchezaji wa Kengold na nitahakikisha ninalipa kila kitu kwa timu hii hadi mwisho wa msimu. Hata kama hatuwezi kubaki Ligi Kuu, nadhani ni muhimu kwetu sisi wachezaji kuonyesha heshima kwa timu yetu na mashabiki wetu," aliongeza Cabaye.

Kwa sasa, Kengold inahesabu za kumaliza msimu kwa heshima katika michezo yao mitatu iliyosalia, dhidi ya Pamba, Simba na Namungo.