Kibaya apeleka kilio Lyon akisawazisha dakika za majeruhi

Muktasari:
Licha wachezaji wengi kupata shida katika mchezo huo kutokana na Uwanja wa Manungu uliopo Turiani Morogoro kuwa na matokeo na kuteleza katika baadhi ya maeneo lakini timu zote zilionekana kushambuliana lakini umakini wa safu za ushambuliaji za timu zote ulikuwa hafifu.
Bao la Jaffary Kibaya dakika ya 93 limewaokoa wenyeji Mtibwa Sugar kuepuka kipigo kutoka kwa African Lyon leo na mchezo huo kumalizika kwa sare ya bao 1-1.
Mtibwa Sugar ilibidi kusubiri mpaka dakika hizo za majeruhi kuweza kusawazisha bao hilo lililowafanya wachezaji wengi wa African Lyon kukaa chini wakishindwa kuamini baada ya mwamuzi kupuliza filimbi ya kumaliza mchezo huo wa Ligi Kuu Bara.
Licha wachezaji wengi kupata shida katika mchezo huo kutokana na Uwanja wa Manungu uliopo Turiani Morogoro kuwa na matokeo na kuteleza katika baadhi ya maeneo lakini timu zote zilionekana kushambuliana lakini umakini wa safu za ushambuliaji za timu zote ulikuwa hafifu.
African Lyon ilikuwa ya kwanza kupata bao dakika ya 61 lililofungwa na kiungo Ramadhan Chombo'Redondo'.
Redondo alifunga bao hilo kwa shuti kali baada ya kuwazidi ujanja mabeki wa Mtibwa Sugar huku kipa Shaban Kado akiwa ametoka golini kuuwahi.
Kutokana na matokeo hayo African Lyon imeendelea kubaki mkiani ikiwa na pointi 20 wakati Mtibwa Sugar imepanda nafasi,mbili hadi nafasi ya 11 baada ya kufikisha pointi 29.