Kikapu Walemavu yasaka Sh35 Milioni kwenda Uswisi

Muktasari:
- Katibu wa Chama Mchezo wa Kikapu cha Watu wenye Ulemavu Tanzania (TWBA), Abdallah Mpogole, aliliambia Mwanaspoti kuwa, fedha hizo zinahitajiwa kwa ajili ya maandalizi na safari hiyo ya Uswisi baada ya timu hiyo kualikwa kwenda kushiriki mashindano hayo ya kimataifa.
TIMU ya Taifa ya mchezo wa Kikapu kwa Walemavu, inahitaji kiasi cha Sh35 Milioni kwa ajili ya safari ya kwenda Uswisi ilikoalikwa kushiriki mashindano ya Kikapu ya 3x3.
Katibu wa Chama Mchezo wa Kikapu cha Watu wenye Ulemavu Tanzania (TWBA), Abdallah Mpogole, aliliambia Mwanaspoti kuwa, fedha hizo zinahitajiwa kwa ajili ya maandalizi na safari hiyo ya Uswisi baada ya timu hiyo kualikwa kwenda kushiriki mashindano hayo ya kimataifa.
Mashindano hayo yamepangwa kufanyika kati ya Julai 1-7 katika jiji la kimataifa la Mies, Uswisi na Mpogole alisema, kati ya fedha hizo, Sh19 milioni zitatumika kwa ajili ya kingilio cha mashindano hayo. Alisema wakiwa kwenye mashindano hayo wachezaji hao watashuhudia pia, fainali ya mashindano ya vijana ya dunia ya umri wa chini ya miaka 19.
Akizungumzia kuhusiana na timu hiyo, alisema inaendelea kujifua, kwenye viwanja vya kituo cha Jakaya Mrisho Kikwete (JMK).
Katika barua iliyotumwa ya mwaliko, imeeleza kila timu inatakiwa iwe na wachezaji 8 wanaume na 8 wanawake, na kila timu inatakiwa icheze michezo 5 kutokana na ukubwa wa timu.
3X3 ni mchezo unaowahusisha wachezaji wanne, wa tatu wakiwa wanacheza ndani ya uwanja na mmoja anakuwa wa akiba
Mchezo unachezwa nusu ya uwanja, na goli linatumika moja, na muda unaotumika ni wa dakika kumi.