Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha Kapilima aachiwa msala KenGold

KAPILIMA Pict

Muktasari:

  • Ofisa Habari na Mawasiliano wa KenGold, Joseph Mkoko aliliambia Mwanaspoti, Kapilima ataendelea kusimamia benchi la timu hiyo kwa michezo iliyobaki msimu huu, kutokana na Heric kutokidhi vigezo vya kuongoza kikosi hicho akiwa kocha mkuu.

KIKOSI cha KenGold kitaendelea kufundishwa na Omary Kapilima kwa michezo iliyobaki, huku Mserbia Vladislav Heric akiwa msaidizi, baada ya kocha huyo aliyetambulishwa Januari 18, mwaka huu kutokidhi vigezo vya kusimamia benchi la ufundi.

Ofisa Habari na Mawasiliano wa KenGold, Joseph Mkoko aliliambia Mwanaspoti, Kapilima ataendelea kusimamia benchi la timu hiyo kwa michezo iliyobaki msimu huu, kutokana na Heric kutokidhi vigezo vya kuongoza kikosi hicho akiwa kocha mkuu.

“Kapilima ndiye kocha mkuu na Heric atakuwa msaidizi wake kutokana na kutokidhi vigezo vya kuliongoza benchi la ufundi, tunaendelea na maandalizi yetu kwa michezo ijayo, ili kuhakikisha tunafanya vizuri kwa ajili ya kusogea juu,” alisema.

KenGold ilianza msimu huu na Kocha, Fikirini Elias aliyekiongoza kikosi katika michezo mitatu na kuchapwa yote kisha Septemba 17, 2024 akaamua kujiweka pembeni mwenyewe, kwa kile alichokieleza kufikia makubaliano ya pande mbili.

Baada ya hapo timu ikaongozwa na Jumanne Challe aliyeipandisha Ligi Kuu Bara kama kocha wa muda kutokana na kutokidhi vigezo vya kusimamia benchi la ufundi kama kocha mkuu na alisimamia michezo mitano, akishinda mmoja tu, sare mmoja pia na kupoteza mitatu.

Oktoba 22, 2024, uongozi wa KenGold ukamtangaza, Omary Kapilima kuiongoza timu hiyo na hadi sasa ameisimamia katika michezo 15, ya Ligi Kuu Bara na kati ya hiyo ameshinda miwili tu, sare sita na kuchapwa saba.

Heric aliyezaliwa Agosti 29, 1966, ana uzoefu mkubwa wa kufundisha timu mbalimbali ikiwemo Club Africain ya Tunisia, Maritzburg United, Polokwane City, FC Cape Town na Chippa United za Afrika Kusini.

Kwa sasa KenGold iko mkiani na pointi 16, baada ya kucheza michezo 23, ikishinda mitatu, sare saba na kupoteza 13, ikikabiliwa na ratiba ngumu ambapo Aprili 3, itaikaribisha Azam FC, huku ikikumbuka mechi ya kwanza ilichapwa kwa mabao 4-1, Oktoba 25, 2024.