Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha Songea United akiri ugumu wa 'Top Four' Championship

MASOUD Pict

Muktasari:

  • Msimu wa 2024-2025, Masoud akiifundisha Stand United, aliiongoza kumaliza nafasi ya tatu Championship na pointi 61, jambo lililoiwezesha kucheza mechi za 'Play-Off' za kusaka tiketi ya kupanda Ligi Kuu Bara, ingawa alikwama.

KOCHA Mkuu wa Songea United ya mkoani Ruvuma, Juma Masoud amesema katika mechi sita za timu hiyo zilizobaki kumalizia msimu huu, ni za kuweka pia heshima kwa sababu ni ngumu kwa kikosi hicho kumaliza nafasi nne za juu.

Akizungumza na Mwanaspoti, Masoud aliyewahi kuifundisha FGA Talents (sasa Fountain Gate), amesema licha ya kuichukua timu hiyo katikati ya msimu, kumekuwa na mabadiliko chanya ya kiuchezaji tofauti na matarajio yake.

"Wakati napewa jukumu hili ilikuwa ngumu kuamini kama tutakuwa na mwenendo mzuri hadi sasa, kwa sababu wachezaji wengi nimewakuta tayari kwenye timu, ila ushirikiano wetu umeonyesha tunaweza kufanya vizuri zaidi," amesema Masoud.

MASO 01

Masoud aliyejiunga na kikosi hicho Januari 2026, akichukua nafasi ya Meja Mstaafu, Abdul Mingange aliyeanza nayo msimu wa 2025-2026, ameshinda mechi saba, sare nane na kupoteza tisa, ikiwa nafasi ya saba na pointi 29.

MASO 02

Msimu wa 2024-2025, Masoud akiifundisha Stand United, aliiongoza kumaliza nafasi ya tatu Championship na pointi 61, jambo lililoiwezesha kucheza mechi za 'Play-Off' za kusaka tiketi ya kupanda Ligi Kuu Bara, ingawa alikwama.