Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

KVZ, JKU na Fufuni zapigana vikumbo kileleni ZPL

ZPL Pict

Muktasari:

  • Baada ya vuta nikuvute ya mzunguko wa 24 wa ligi hiyo ulioanza Mei Mosi hadi Mei 4 mwaka huu, KVZ imerudi kileleni ikikusanya pointi 49 baada ya kuisulubu Muembe Makumbi mabao 3-1.

ULE msemo wa haiishi mpaka iishe unaanzia hapa kwa timu tatu zilizopo juu ya msimamo wa Ligi Kuu Zanzibar ambazo ni KVZ, JKU na Fufuni zilizotofautiana pointi moja tu.

Baada ya vuta nikuvute ya mzunguko wa 24 wa ligi hiyo ulioanza Mei Mosi hadi Mei 4 mwaka huu, KVZ imerudi kileleni ikikusanya pointi 49 baada ya kuisulubu Muembe Makumbi mabao 3-1.

Kabla ya hapo, JKU ilifanikiwa kupanda kileleni mwa msimamo baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya New King, lakini ushindi wa KVZ juzi ukairudisha timu hiyo nafasi yake, huku JKU ikibaki ya pili na pointi 48.

Kwa upande wa Fufuni iliyopanda daraja msimu huu, imeendelea kuonyesha makali yake kwa kuitandika Chipukizi mabao 2-0 na kufikisha pointi 47 ikiwa nafasi ya tatu.

Kutokana na msimamo ulivyo, bado imekuwa ngumu kutabiri timu itakayokuwa bingwa wa Ligi Kuu Zanzibar msimu huu kwa sababu ya tofauti ya alama chache zaidi zilizopishana, huku zikibaki mechi sita kwa kila timu.

Ukistaajabu hayo, utakutana na New Stone Town iliyokwishashuka daraja ambapo licha ya hivyo, imepata ushindi wa pili katika ligi baada ya kuichapa Junguni United mabao 3-2 na kufikisha alama sita kati ya michezo 24 iliyocheza.

Junguni nayo imeshuka daraja na kuzifanya timu hizo mbili kutokea Pemba msimu ujao kushiriki Ligi Daraja la Kwanza, hivyo zinasubiriwa mbili kuungana nazo kutimiza idadi ya timu nne, huku Wembe kutoka Pemba na Black Sailors ya Unguja zikikata tiketi ya kushiriki Ligi Kuu Zanzibar msimu ujao kutokea Ligi Daraja la Kwanza.